MADIWANI MANISPAA YA SHINYANGA KUSHIRIKIANA NA AGAPE KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WASICHANA KWENYE MASOKO



Shirika la Agape Aids Control Program la mkoani Shinyanga, limehitimisha kikao na madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga, kilichokuwa na lengo kujadili namna ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana kwenye masoko ambapo kwa pamoja wameweka mikakati mbalimbali ili kutokomeza ukatili kwenye masoko yaliyopo katika manispaa hiyo.



Kikao hicho kimefanyika siku mbili kuanzia Oktoba 30-31,2019 kwenye ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Katemi Shinyanga mjini, na kuhudhuriwa pia na viongozi wa Masoko Sita ya Shinyanga mjini, pamoja na Maofisa Maendeleo na ustawi wa jamii manispaa na mkoa.

Wakiwasilisha maazimio yao kwenye kikao hicho wameahidi kwenda kutoa elimu kwenye masoko juu ya kupinga ukatili huo, utungwaji wa sheria ndogo, pamoja na kuhamasisha utengwaji wa bajeti kwenye halmashauri ili kusaidia mpango mkakati wa taifa wa serikali wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto MTAKUWWA uweze kufanikiwa kwa asilimia 100. 

Akizungumza wakati  wa kuhitimisha kikao hicho Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo la Agape John Myola, amesema wamefanya kikao hicho na waheshimiwa madiwani, ambao ndiyo watunga Sheria za manispaa ya Shinyanga, ili kuona namna watakavyoshirikiana kwa pamoja kutokomeza ukatili kwenye masoko.

Amesema katika utekelezaji wa mradi wao wa “Mpe Riziki si Matusi” ambao unafadhiliwa na Shirika la kimataifa la UN WOMEN kupitia shirika la Equality for Growth (EFG), wamedhamiria kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana kwenye masoko sita ya manispaa ya Shinyanga ambayo ni Kambarage, Soko kuu, Nguzonane, Ngokolo, majengo mapya, na Ibinzamata.

“Tumefanya kikao hiki na madiwani wa manispaa ya Shinyanga ambao ndiyo watunga Sheria za manispaa, ili kujadiliana kwa pamoja kuona namna tukavyo shirikiana kutokomeza ukatili wa wanawake na wasichana kwenye masoko yetu ya manispaa ya Shinyanga, ikiwamo kuondoa lugha chafu za matusi, dhuluma, kushikwa maumbile yao, kutakwa kimapenzi kwa nguvu pamoja na vipigo,” amesema Myola.
 Naye Afisa mradi huo wa kutokomeza ukatili masokoni wa ‘Mpe Riziki Si Matusi’ Helena Daudi, amesema Mradi huo umeanza kutekelezwa tangu mwaka jana Novemba 2018 ambao unakoma mwaka huu Oktoba 2019, ambapo mpaka sasa wamefanikiwa kupunguza ukatili huo kwa kiwango kikubwa.

Amesema matarajio yao ya kikao hicho cha madiwani pamoja na wenyeviti wa masoko ni kuona namna wakavyofanya kazi kwa vitendo pamoja na kutekeleza maadhimio yao waliyojiwekea kwenye kikao hicho, na kutokomeza kabisa ukatili masokoni.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI


Mkurugenzi wa Shirika la Agape John Myola akizungumza kwenye kikao na madiwani wa manispaa ya Shinyanga, viongozi wa Masoko, Maofisa maendeleo, na Ustawi wa jamii namna ya kushirikiana kwa pamoja kwenda kufanya kazi ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana kwenye Masoko. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Mkurugenzi wa Shirika la Agape John Myola, akisisitiza wajumbe wa kikao hicho kwenda kutekeleza maazimio yao vyema ili kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana kwenye Masoko ya Shinyanga Mjini.

Afisa mradi wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana kwenye Masoko ya Shinyanga Mjini Helena Daudi, akizungumza wakati wa kuhitikisha kikao hicho cha siku mbili na kusisitiza utendaji kazi kwa vitendo ili ukatili usiwepo tena sokoni.

Meneja miradi kutoka Shirika la Agape Peter Amani akizungumza kwenye kikao hicho cha kupinga ukatili dhidi ya wanawake na wasichana kwenye Masoko ya Shinyanga Mjini.

Afisa wa dawati la jinsia kutoka Jeshi la Polisi wilaya ya Shinyanga Lilian Charles akiwasilisha mada ya ukatili, kwenye kikao hicho.

Mratibu wa dawati la kuzuia ukatili kwenye Masoko ya Shinyanga Enjel Mwaipopo akizungumza kwenye kikao hicho na kuomba yale yote yaliyojadiliwa yakafanyiwi kazi.

Wajumbe wakiwa kwenye kuhitimisha kikao na Shirika la Agape namna ya kwenda kufanya kazi ya kushikamana pamoja katika kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana kwenye masoko ya Shinyanga.

Wajumbe wakiendelea na kikao.

Wajumbe wakiendelea na kikao.

Wajumbe wakiendelea na kikao.

Wajumbe wakiendelea na kikao.

Wajumbe wakiendelea na kikao.

Wajumbe wakiendelea na kikao.

Wajumbe wakiendelea na kikao.

Wajumbe wakiendelea na kikao.

Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga John Kisandu akichangia mada kwenye kikao.

Diwani wa viti maalumu manispaa ya Shinyanga Zena Gulamu akichangia mada kwenye kikao.

Diwani wa Kata ya Lubaga manispaa ya Shinyanga Obed Jilala akichangia mada kwenye kikao.

Diwani wa Kata ya Kitangili manispaa ya Shinyanga Hamis Ngunila akichangia mada kwenye kikao.

Diwani wa Kata ya Masekelo Samweli Sambaye akichangia mada kwenye kikao.

Mwenyekiti wa Soko kuu mjini Shinyanga Alex Steven akichangia mada kwenye kikao.

Kaimu mwenyekiti wa Soko la Nguzonane Hilda Athanas akichangia mada kwenye kikao.

Katibu wa Soko la Majengo Mapya Zacharia James akichangia mada kwenye kikao.

Afisa ustawi wa jamii mkoa wa Shinyanga Lydia Kwesigabo akichangia mada kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kazi ya vikundi.

Wajumbe wakiwa kwenye kazi ya vikundi.

Wajumbe wakiwa kwenye kazi ya vikundi.

Diwani wa Kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga Emmanuel Ntobi akiwasilisha kazi ya kikundi cha Madiwani.

Afisa maendeleo Kata ya Mjini Tully Kamwela, akiwasilisha kazi ya kikundi cha maofisa maendeleo na Ustawi wa jamii.

Katibu wa Soko la Majengo Mapya Zacharia James akiwasilisha kazi ya kikundi ya viongozi wa Masoko ya Shinyanga.

Picha na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post