Watu nane wamefariki dunia wilayani Handeni mkoani Tanga, baada ya gari walilokuwa wanasafiria, kutumbukia mtoni kutokana na daraja kukatika.
Akizungumza na MwanaHALISI Online kwa njia ya simu, leo tarehe 26 Oktoba 2019, Edward Bukombe, Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, amesema anafuatilia tukio hilo.
Kamanda Bukombe amesema yuko njiani kuelekea eneo la tukio, na kwamba atatoa taarifa kamili kuhusu tukio hilo, pindi atakapofika eneo la tukio.
“Hizo taarifa nimezipata na sasa hivi niko barabarani naelekea eneo la tukio, nikifika nitawajulisha kilichotokea. Maana kwa sasa niko mbali na tukio,” amesema Kamanda Bukombe.
Chanzo- Mwana Halisi Online
Social Plugin