ASILIMIA 15 YA MAPATO YA KOROGWE MINI MARATHON KUSAIDIA WAATHIRIKA WA MAFURIKO WILAYANI KOROGWE

MKUU wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga Kisa Gwakisa katikati kikimbia pamoja na Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi kulia wakikimbia mbio za kilomita 5 za Korogwe Mini Marathon zilizofanyika leo mjini Korogwe 
Wakimbiaji wa Baiskeli wakiwa wameanza mbio zao kwenye Mashindano ya Korogwe Mini Marathon 


Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa kulia akikimbia kilomita 5 wakati wa Mashindano ya Korogwe Mini Marathon leo mjini Korogwe
Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi kulia akivalishwa medali na Mratibu wa Mashindano ya Korogwe Mini Marathon Juma Mwajasho mara baada ya kumaliza mbio za kilomita 5
Mratibu wa Mashindano ya Korogwe Mini Marathon Juma Mwajasho 
 Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi kulia akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa mashindano ya Korogwe Mini Marathon kwa upande wa wanaume aliyekimbia kilomita 10 Jumanne Ndege kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Korogwe Michael John ambaye ni Afisa Tarafa ya Korogwe
 Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akiendelea kutoa zawadi kwa washindi mbalimbali mara baada ya kumalizika mashindano hayo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa 
 Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akiendelea kutoa zawadi kwa washindi mbalimbali mara baada ya kumalizika mashindano hayo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Korogwe Michael John ambaye ni Afisa Tarafa ya Korogwe 
 Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akizungumza wakati wa mashindano ya Korogwe Mini Marathon 
 MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa akizungumza wakati wa mashindano ya Korogwe Mini Marathon

 MKUU wa wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa kushoto akimpongeza Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi 
 Sehemu ya wananchi wakifuatilia mbio hizo
 MKUU wa wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa katikati akiwa pamoja na washiriki wengine waliojitokeza kushiriki mashindano ya Korogwe Mini Marathon kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Timotheo Mzava
NA MWANDISHI WETU, KOROGWE

ASILIMIA 15 ya mapato yanayotokana na mashindano ya Riadhaa ya Korogwe Mini Marathon yanatarajiwa kutumika kwenye kuwasaidia waathirika wa mafuriko wilayani Korogwe ambao wamekumbwa na majanga mbalimbali.

Hayo yalisemwa leo na Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa wakati wa mashindano ya Riadhaa ya Korogwe Mini Marathon yaliyofanyika mjini Korogwe na kuhudhuriwa na washiriki kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.

Alisema maafa hayo ni makubwa kutokana na wamewaacha baadhi ya wananchi wakikosa makazi huku wengine wakipoteza maisha hivyo wameona watumie nafasi hiyo kuwafariji wananchi hao kwa kuwapatia kiasi hicho. 


“Ndugu zangu Korogwe tumekumbwa na maafa wenzetu wamepoteza maisha maji yamekata barabara kwa kutumia Mashindano hayo ya Korogwe Mini Marathon tutatoa asilimia 15 kuwasaidia ndugu zetu waliopata maafa na mvua hizo kuwapa mkono wa Pole kwa kuwa ni watanzania wenzetu”Alisema DC Kissa. 

Aidha alisema kwamba lengo kuu la mashindano hayo ni kumuenzi baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ikiwa leo ni mwaka 2019 anafikisha miaka 20 wao wana Korogwe tunatumia siku hii kwa kuenzi kwa kufanyika mashindano hayo”Alisema

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba Korogwe wameungana na dunia nzima kumuenzi baba wa Taifa ambayo aliwaachia watanzania demokrasia ya vyama vingi kitu ambacho kinaendeleza kwa vitendo na Rais Dkt John Magufuli.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba lengo la pili ni kuchangia miundombinu ya elimu kupitia kampeni ya Nivushe kuhakikisha wanasukuma mbele gurudumu la maendeleo ya sekta hiyo. 

“Lakini pia tunawashukuru Tanapa wametuchangia milioni 30, tunawashuiru marathon hii isingekamilika kama sio wadau hawa wameweza kudhamini huku mdhamini wa kwanza akiwa Tanapa, wa pili ni Gomba, wa cyclyn ...Lakini Tunawashuku pia NMB na CRDB tunategema kipindi kijacho tutakuwa na ongezeko la wadhamini “Alisema.

Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaume waliokimbia kilomita 10 alikuwa ni Jumanne Ndege kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) mkoani Arusha ambaye alikimbia dakika 30 na sekunde 7 ambaye alizawadiwa medali na kitita cha laki mbili.

Nafasi ya mshindi wa pili ilikwenda kwa Jackson Makombe ambaye alikimbia dakika 31 na sekunde 04 ambaye pia akitokea JKT Mkoani Arusha aliyepata kitita cha 140,000 huku mshindi wa tatu ikienda kwa Charles Sule ambaye alikimbia umbali wa dakika 32 na sekunde 07 ambaye pia alitokea JKt mkoani Arusha alizawadiwa kitita cha sh.80,000.

Kwa upande wa wanawake kilomita mshindi wa kwanza ilichukuliwa na Grace Jackson kutoka klabu ya JKT Mkoani Arusha ambaye alikimbia kwa kutumia dakika 35 na sekunde 51 ambaye alipata kitita cha sh.200,000,nafasi ya pili ikichukuliwa na Banuelia Bryson kutoka mkoani Kilimanjaro ambaye alikimbia dakika 41 na sekunde 16 aliyepata kitita cha sh.140,000,huku mshindi wa tatu ikichukuliwa na Pendo Pamba kutoka Klabu ya JKT ya Mkoani Arusha akikimbia kwa dakika 42 na sekunde 18 akizawadiwa kitita cha 80,000.

Hata hivyo kwa upande wa mbio za Baiskeli kilomita 30 wanaume mshindi wa kwanza aliibuka Boniface Saimoni kutoka mkoani Simiyu ambaye alikimbia dakika 49 na sekunde 59 na kupata kitita cha sh.200,000,huku mshindi wa pili ikichukuliwa na Mussa Makala aliyepata kitita cha sh.160,000,na mshindi wa tatu ikichukuliwa na Rashid Ally akizawadiwa kitita cha sh.120,000.

Kwa upande wa mbio baiskeli wanawake kilomita 20 mshindi wa kwanza ilichukuliwa na mshindi wa pili ni Anna Pimax huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa

Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi hizo mgeni rasmi wa mashindano hayo Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi alimpongeza Mkuu huyo wa wilaya kwa kubuni na kuanzisha mashindano hayo ambayo yamekuwa na tija kubwa. 

Alisema licha ya kuwepo kwa changamoto ya mvua lakini mashindano hayo yamefana na kuwa kivutio kikubwa kwa wananchi na wana michezo ambao walijotokeza kushuhudia mashindano hayo. 

“Lakini pia nipongeze kamati ya maandalizi kwa kufanikisha dhumuni hili kubwa ikiwa ni kumuenzi baba wa Taifa ambapo kesho ni kumbukizi yake lakini pia kutumia fursa hiyo kuhamamsisha wananchi kuajiandikisha”Alisema

Mwisho.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post