Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa orodha ya majina ya wanafunzi 11,378 wa mwaka 2019/2020 waliopata mkopo wa awamu ya pili.
Mkurugenzi mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru ametoa taarifa Jumamosi Oktoba 26, 2019 na kubainisha kuwa waliopata mikopo hadi sasa ni 42,053 wa mwaka wa kwanza. Amesema mkopo waliopata ni sawa na Sh148,56 bilioni.
Badru amesema mwaka 2019/20, Serikali imetenga Sh450 bilioni kwa ajili ya wanafunzi 128,285.
Amebainisha kuwa kati ya wanafunzi hao, zaidi ya 45,000 ni wa mwaka wa kwanza na 83,285 ni wanafunzi wenye mikopo wanaoendelea na masomo.