Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM – Taifa), Philip Mangula ametoa tamko la azimio la chama hicho juu ya vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa Zimbabwe tangu mwaka 2000.
Mangula ametoa tamko hilo leo Jumatano Oktoba 24, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salam ambapo amesema kuwa vikwazo hivyo ni mwendelezo wa fikra na matendo ya unyojaji kwa Afrika na hivyo wameazimia kuwa uonevu huo ufike mwisho.
“Kwa kutambua jukumu letu katika kuimarisha umoja, ushikamano wa Waafrika na kuendeleza mapambano dhidi ya ukoloni mamboleo pamoja na kuimarisha uhusiano mwema wa vyama vya siasa vya nchi nyingine vyenye itikadi kama ya CCM, chama kinaamini kuwa vikwazo dhidi ya watu wa Zimbabwe ni muenedelezo wa fikra na matendo ya unyojaji kwa Afrika na sasa tuaazimia kuwa uonevu huo ufike mwisho,”.
“Ni miaka 19 ya kuwekewa vikwazo hata wale ambao walikuwa hawajazaliwa wanaadhibiwa na vikwazo hivi nadhani huu sio ubinadamu, sambamba na kutekeleza maamuzi hayo CCM kwa nafasi yake ya kuwa chama kiongozi wakati wote wa kulikomboa Bara la Afrika kisiasa inatumia nafasi hii kupaza sauti na kushinikiza mataifa yote yaliyoiwekea vikwazo Zimbabwe kuviondoa bila masharti yoyote ili nchi hiyo iweze kupiga hatua za haraka za maendeleo kiuchumi na kijamii kwa watu wake,” amesema Mangula.
Aidha Mangula amevitaka Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika na watu wote wenye mapenzi mema kuendelea kupaza sauti hadi pale Zimbabwe itakapoondolewa vikwazo hivyo vya kiuchumi ambavyo havizingatii ubinadamu.
Social Plugin