Picha : MKUU WA MKOA WA SHINYANGA AZINDUA CHANJO YA SURUA, RUBELLA NA POLIO



Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, amezindua Kampeni ya kitaifa ya Chanjo ya Surua, Rubella na Polio, mkoa wa Shinyanga ambayo itatolewa kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano ili kuwapatia kinga dhidi ya magonjwa hayo.


Uzinduzi wa chanjo hiyo umefanyika leo Oktoba 17, 2019 katika kata ya Lyabukande halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, na kuhudhuriwa na wananchi wa kata hiyo pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo wataalamu wa afya ngazi ya mkoa na wilaya.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo Telack amesema, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. John Magufuli, inathamini afya za wananchi wake hasa katika kuzuia magonjwa yanayozuilika kwa chanjo na ndiyo maana chanjo hiyo inatolewa bure.

“Nawaombeni wazazi wote mkoani Shinyanga mjitokeze kwa wingi kupeleka watoto wenu wenye kuanzia umri wa miezi tisa hadi 49 yaani miaka Minne na miezi 11 kupatiwa chanjo hii ya Surua, Rubella na polio ili kuwapatia kingi dhidi ya magonjwa haya”,amesema Telack.

“Ugonjwa wa Surua una madhara makubwa kwa watoto ambapo unaweza kumsababishia madhara ya upofu, kuhara, na utapiamlo, Rubela unaweza kumsabishia mtoto ulemavu, magonjwa ya moyo na mtoto wa jicho, Polio unaweza kumsabishia mtoto kupooza mwili wote, hivyo nawataka wazazi msipuuzie zoezi hili,”ameongeza.

Pia amewaonya wananchi ambao watapotosha zoezi hilo la utoaji chanjo kwani baadhi yao wamekuwa na tabia ya kufanya upotoshaji, na kubainisha kuwa atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Naye Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume, ametaja takwimu za watoto ambao watapewa chanjo hiyo kwa mkoa mzima kuwa ugonjwa wa Surua na Rubella watafikiwa watoto 286,124 na Polio watoto 151,547.

Amesema zoezi hilo limeanza leo Oktoba 17 na litakoma tarehe 21 mwaka huu, ambapo huduma hiyo itatolewa kwenye maeneo yote ya huduma za afya mkoa wa Shinyanga.

Nao baadhi ya wazazi ambao walifika kwenye uzinduzi huo wa chanjo, pamoja na watoto wao kuanza kupatiwa chanjo hiyo akiwamo Monica Shija, wameipongeza Serikali kwa kujali afya za watoto wao na kuwapatia kinga.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza wakati akizindua chanjo ya Surua, Rubella na Polio leo Alhamis Oktoba 17,2019 katika kata ya Lyabukande halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Chanjo hiyo itatolewa kwa watoto waliochini ya umri wa miaka mitano. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack, akionya wananchi kuacha kupotosha juu ya utolewaji wa Chanjo ya Surua, Rubella na Polio.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akitoa wito kwa wazazi kujitokeza kwa wingi kupeleka watoto wao waliochini ya umri wa miaka mitano kupatiwa Chanjo ya Surua, Rubella na Polio.

Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya Surua, Rubella na Polio namna itakavyo saidia kukinga watoto dhidi ya magonjwa hayo.

Mwananchi Monica Shija akiishukuru serikali kwa kutoa chanjo ya Surua, Rubella na Polio.

Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack, akizindua chanjo ya Surua, Rubella na Polio kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.

Dkt. Geofrey Anthony akitoa chanjo ya Surua, Rubela na Polio kwa mtoto.

Muuguzi wa Zahanati ya Lyabukande Godfrey Mbelela (kulia), akitoa maelezo kwa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe.Zainabu Telack namna watakavyotoa huduma ya chanjo ya Surua, Rubella na Polio.

Wananchi wakiwa na watoto wao kwenye uzinduzi wa chanjo ya Surua, Rubella na Polio.

Wananchi wakiwa na watoto wao kwenye uzinduzi wa chanjo ya Surua, Rubella na Polio.

Wananchi wakiwa na watoto wao kwenye uzinduzi wa Chanjo ya Surua, Rubella na Polio.

Wananchi wakiwa na watoto wao kwenye uzinduzi wa Chanjo ya Surua, Rubella na Polio.

Wananchi wakiwa na watoto wao kwenye uzinduzi wa Chanjo ya Surua, Rubella na Polio.

Wananchi wakiwa na watoto wao kwenye uzinduzi wa Chanjo ya Surua, Rubella na Polio.

Wananchi wakiwa na watoto wao kwenye uzinduzi wa Chanjo ya Surua, Rubella na Polio.

Kikundi cha sanaa cha Shinyanga kikitoa Burudani kwenye uzinduzi wa Chanjo ya Surua, Rubella na Polio.

Awali Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiwasili kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Chanjo ya Surua, Rubella na Polio, kwenye Kata ya Lyabukande halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akipiga picha ya pamoja na baadhi ya wazazi waliopeleka watoto wao kupatiwa Chanjo ya Surua, Rubella na Polio, wa kwanza kulia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, na wakwanza mkono wa kushoto ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba.

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post