Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Katika jitihada za kukuza na kuieneza lugha ya Kiswahili,Chuo kikuu cha Dar es Salaam mapema mwezi January mwaka 2020 kinatarajia kuanza kutoa mitihani ya kimataifa ya ujuzi wa lugha hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari hii jana Jijini Dodoma,Katibu mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dkt.Leonard Akwilapo amesema kuwa katika awamu hii wameona mafanikio makubwa katika kuiendeleza
lugha ya Kiswahili kwani sasa imekuwa moja kati ya lugha rasmi za Jumuiya ya nchi za kusini mwa Afrika yaani SADC
Dkt.Akwilapo ameongeza kuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitakuwa ndio Chuo kikuu cha kwanza Duniani kutunga mitihani hiyo,kusimamia udahiri na usahihishaji wake na kutoa cheti cha kimataifa kinachoonesha kiwango cha ujuzi wa mtahiniwa ambapo pia ametabainisha walengwa wa mitihani hiyo
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtanzania kutoka Taasisi ya Confucius,Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Mgoda Mutembei yeye amesema kuwa kuna wananfunzi wengi wanaosoma lugha ya Kiswahili nje ya nchi na wangependa kutambulkika kuwa wamesoma lugha hiyo kwa kuwa na cheti
maalumu hivyo Chuo kikuu cha Dar es Salaam kitakuwa ni suluhisho katika suala hilo.
Dkt.Akwilapo pia ameuhakikishia umma kuwa tayari kuna makubaliano baina ya walimu wa Kiswahili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na walimu wanaofundisha kiswahili katika vyuo vya nje kuhusiana na mitihani hiyo
Social Plugin