MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa waandikishaji na waandaaji wa orodha ya wapiga kuwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019 ambapo aliwataka wawe makini ili wasijikute wameingia matatani kulia ni Afisa Tarafa ya Korogwe Michael John kushoto ni Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Korogwe mji Kassim Kaoneka.
Afisa Tarafa ya Korogwe Michael John akizungumza kwenye mafunzo hayo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa
Mwanasheria wa Halamshauri ya Korogwe mji Mwanasheria wa Halmashauri ya Korogwe mji Madgalena John akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Korogwe mji Kassim Kaoneka akizungumza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa
Sehemu ya waandikishaji na waandaaji wa orodha ya wapiga kura Korogwe wilayani Korogwe wakiwa kwenye mafunzo hayo
Sehemu ya waandikishaji na waandaaji wa orodha ya wapiga kura Korogwe wilayani Korogwe wakiwa kwenye mafunzo hayo
MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa kushoto akiagana na Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Korogwe mji Kassim Kaoneka mara baada ya kufungua mafunzo hayo katikati ni
MKUU wa
wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga Kissa Gwakisa amewaonya waandikishaji na
waandaaji wa orodha ya wapiga kura wilayani humo watakaobainika kuwaingiza raia
wa kigeni kwamba hawatasalimika badala yake watashughulikiwa kwa mujibu wa
sheria.
DC Kissa
aliyasema hayo leo wakati akifungua mafunzo kwa waandikishaji na waandaaji wa
orodha ya wapiga kuwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019 ambapo
aliwataka wawe makini ili wasijikute wameingia matatani.
Alisema
kwamba pamoja na kuwepo kwa mafunzo hayo lakini wapo baadhi ya waandikishaji na
waandaaji wa orodha ya wapiga kura kwenye uchaguzi huo wanaweza kufanya tofauti
na maelekezo hivyo watahakikisha wanashughulikiwa kwa mujibu wa sheria
zilizopo.
“Ndugu
zangu wasimamizi uchaguzi wilayani, wanasimamia uchaguzi wasaidizi ngazi ya
wilaya, Kata, Vijini na Mitaa kuhakikisha wanakuwa waaminifu na nidhamu wakati
wa kutekeleza majukumu yenu na hii itasaidia kuepusha malalamiko huku akiwaonya
watakaokwenda kunyume watachukuliwa hatua kali dhidi yao “Alisema DC Korogwe.
Aidha Mkuu
huyo wa wilaya aliwataka wasimamizi hao kuwa mfano mzuri katika utekelezaji wa
majukumu yao kwa kuhakikisha wanatenda haki ili uchaguzi uweze kwenda kwa haki
na usalama bila kuwepo na malalamiko ya aina yoyote ile.
“Lakini pia
niwaambie kwamba elimu hii muende kuitoa na ngazi za chini..kupiga kura ni haki
ya kila mtanzania hivyo tunawategemea kama Taifa kundi hili lipo kila kila
wilaya kwa nyie wa hapa nataka kuona mfano mzuri Korogwe Uchaguzi uende vizuri
kusiwe na malalamiko”Alisema DC Kissa.
Hata hivyo
alisema kwamba wataendelea kupewa semina ili kuweza kuwasaidia kuondokana na
kufanya makosa kwenye uchaguzi huo ikiwemo kuzingatia nidhamu ya hali ya juu
wakati mkitekeleza majukumu yenu mapya.
“Mpo kwenye
nafasi nyeti Taifa linawategemea yale mambo siri mfanye siri lazima mtambua
kwamba mnajukumu kubwa na zito kwa watanzania lakini mkizingatia maelekezio mnayopewa
itakuwa chachu kubwa ya kusimamia vema uchaguzi bila kuwepo wa manunguniko”Alisema
Mkuu huyo wa wilaya.
Awali
akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo Mwanasheria wa Halmashauri ya Korogwe
mji Madgalena John alimuhaidi Mkuu huyo wa wilaya kwamba hawatamuangusha wala
kuiangusha serikali na watakwenda kuitendea haki serikali yao na wananchi wa
wilaya hiyo.
Alisema
kwamba wanakwenda kufanya jukumu hilo nzito ambalo wamekabidhiwa na
serikali na wanaimani baada ya neno
kutoka kwake limewapa mwanga mpya ambao utakuwa chachu katika kutekeleza
majukumu yao .
“Nikuhaidi
Mh DC hatutakuangusha wewe wale serikali tutakwenda kuitendea haki serikali na
wananchi wa korogwe jukumu hilo zito lakini tutalifanya kwa ufanisi mkubwa “Alisema
.