Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Imeelezwa kuwa kufuta matokeo ya Mtihani mmoja wa shule ya msingi ni Sawa na kupata hasara ya Upotevu wa Bilioni 100.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Dkt Charles Msonde amebainisha hayo jijini Dodoma katika kikao kilichokutanisha Maafisa wa Baraza la Mitihani Tanzania pamoja na Chama Cha Walimu Tanzania[CWT]Wenye lengo la kujadili na kutathimin namna bora ya kuendelea kudhibiti ufujaji wa mitihani hapa nchini.
Dkt.Msonde amesema Mwalimu ni afisa muhimu katika udhibiti ufujaji mitihani lakini anapojihusisha na wizi wa mitihani hiyo ni kujidhalilisha taaluma yake hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuwa mnyenyekevu na mwadilifu kwa maslahi ya nchi yake katika kuhakikisha ufujaji wa mitihani haitokei ili kuweza heshima na hadhi ya mitihani kwani hukumika gharama kubwa katika uandaaji wa mitihani.
Aidha, Dkt Msonde amesema wamekwisha kuhakiki jumla ya watumishi laki tano na kumi na mbili na mia saba sabini na saba ambapo watumishi elfu kumi na tano na mia nne kumi na moja wamebainika wameghushi vyeti.
Katika hatua nyingine Dkt.Msonde amesema Baraza la Mitihani Tanzania ndio Baraza pekee linaloongoza barani Afrika kwa utendaji kazi mzuri ambao hudhibiti wa ufujaji wa mitihani upo kiwango cha juu ndio maana nchi mbalimbali barani Afrika huja kujifunza nchini Tanzania namna baraza hilo linavyofanya kazi.
Hivyo,Dokta.Msonde ametumia fursa kukipongeza chama cha Walimu Tanzania CWT,pamoja na wadau wa elimu kwa ujumla wakiwemo walimu kwa kuendelea kuwa wanyenyekevu na kuonesha uzalendo mzuri katika kudhibiti ufujaji wa mitihani.
Kwa upande wa Rais wa Chama cha walimu Tanzania Mwalimu Leah Ulaya Pamoja na katibu Mkuu wa Chama cha walimu Tanzania CWT Komred Mwalimu Deus Seif Wamesema ni vyema serikali ikaangalia vyema suala la kupandisha vyeo pamoja na madaraja kwani walio wengi wamekuwa wakipandishwa huku mshahara ukiwa palepale.
Kwa upande wao,walimu waliobahatika kuhudhuria katika kikao hicho wamesema semina na mafunzo mbalimbali waliyoyapata yatawasaidia kuendelea kuwa na nidhamu,uzalendo katika taaluma zao.
Social Plugin