Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo amezitaka Halmashauri 31 zenye ofisi nje ya maeneo ya utawala kuhamia katika maeneo hayo katika kipindi cha siku 30 kuanzia leo Jana Jumatatu Oktoba 7, 2019.
Taarifa iliyotolewa na mkuu wa kitengo cha mawasiliano Serikali Tamisemi, Rebecca Kwandu inaeleza kuwa Jafo ametoa agizo hilo jana mkoani Rukwa baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa Rais wa Tanzania, John Magufuli kuhusu halmashauri hizo.
Amesema halmashauri itakayozembea kutekeleza agizo hilo itafutwa.
Social Plugin