Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Kissa G. Kasongwa wametembelea eneo la Mandera linalounganisha wilaya za Korogwe na Handeni na kujionea mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa na kusababisha barabara kuu kutoka Dar es salaam kwenda Mikoa ya kaskazini kufungwa kwa muda
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi (aliyesimama mbele kushoto) akizungumza na baadhi ya wananchi alipotembelea kuona athari za mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa na kusababisha barabara kuu kutoka Dar es salaam kwenda Mikoa ya kaskazini kufungwa kwa muda, kulia mbele ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Kissa G. Kasongwa. Octoba 13,2019
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Kissa G. Kasongwa.(Kulia mbele) akiwapa pole wakazi wa wilaya ya Korogwe pamoja na wananchi wote walioshindwa kuendelea na Safari kutokana na maji kujaa katika eneo hilo la Mandera kushoto mbele ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi
Hili ndilo eneo la Mandera ambapo daraja lilifungwa kwa muda
Maji yakiwa yamezidi daraja , ingawa hapa maji yanaonekana kupungua kiasi
Hali ya mafuriko ilivyokuwa katika eneo la Mandera
Mhe. Kissa G. Kasongwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe (wa tatu kutoka kushoto) akimonesha jambo Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi walipotembelea eneo la mafuriko.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akisisitiza jambo walipotembelea eneo la mafuriko.
Picha na Fredy Njeje - Korogwe