Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti
Na Lydia Lugakila - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti ametoa siku 3 kwa Halmashauri ya Bukoba Mkoani Kagera kuhamia katika eneo jipya la Bujuna ngoma lililopo katika kata ya Kemondo ili waweze kutoa huduma kwa wananchi wakitokea katika eneo hilo.
Mkuu wa mkoa wa Kagera Bligedia Jenerali Gaguti ametoa Agizo hilo jana Oktoba 21, 2019 katika kikao cha kamati ya Ushauri ya mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa mkoa huo uliopo katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.
Mhe. Gaguti amesema tayari uongozi wa Halmashauri umeandikiwa barua kwa ajili ya kuhamia eneo hilo ambapo amewataka viongozi hao wa Halmashauri kuanza upya mchakato wa kutafuta eneo jipya la makao makuu ya Halmashauri kwa kuwashirikisha wananchi ,wadau, pamoja na viongozi kwani ndiyo watakuwa watumiaji wa mamlaka hayo.
Amesema madiwani ni sehemu ndogo ya maamuzi ya kuhamisha Halmashauri ikiwa mchakato huo unapaswa kurudi kwa wadau ili waweze kupendekeza eneo litakalohudumia watu wengi kama malengo yaliyokusudiwa.
"Natoa siku tatu huduma lazima zianze kutolewa kutokea makao makuu ya halmashauri ya wilaya ya Bukoba mpango huo uwe shirikishi kwa kina", Gaguti.
Agizo hilo limetolewa ikiwa zimepita siku tano za baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo kupitisha eneo la kata ya Kemondo kuwa makao makuu ya Halmashauri hiyo.
Hata hiyo akitoa matokeo ya upigaji wa kura ya kuchagua eneo la kuhamia , mwenyekiti wa halmashauri hiyo Murshid Ngeze alisema maeneo yaliyokuwa yamependekezwa ni matatu ambapo eneo la kwanza lilipata kura moja, la pili kumi na sita na eneo la Bujuna ngoma lililopo katika kata ya Kemondo kupata kura 22.
Social Plugin