Wakazi wa eneo la Kapset kaunti ya Bomet nchini Kenya wamepigwa na butwaa kufuatia kisa cha jamaa kufariki dunia baada ya kunigwa na kipande cha maini.
Inasemekana marehemu aliyetambulika kwa jina la Samuel Towett aliingia katika bucha moja iliyoko eneo hilo na kumuagiza mhudumu kumuuzia nyama, maini na utumbo.
Polisi walisema marehemu alibugia kipande cha ini na kukila wakati mhudumu wa bucha akimpimia nyama.
Inasemekana alipokea huduma ya kwanza kabla ya kukimbizwa katika zahanati ya Itare Forest ambapo ilitangazwa kuwa tayari alikuwa amekata roho.
Madaktari walisema marehemu alifariki akiwa njiani.
Hata hivyo, wakati maafisa wa polisi walipowasili katika zahanati hiyo walikuta tayari jamaa wa marehemu wamepashwa habari na kuundoa mwili wake katika zahanati hiyo.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha maiti cha hospitali ya Kapkatet huku familia yake ikiendelea na mipango ya mazishi.
Via Tuko
Social Plugin