Mwanafunzi bora kitaifa kwa upande wa wavulana katika mtihani wa darasa la saba 2019, Francis Hussein Gwagi amesema anataka kuwa mwanafunzi bora mitihani ya sekondari kama ilivyokuwa shule ya msingi.
Mtoto huyo aliyehitimu Shule ya Msingi Paradise wilayani Chato mkoani Geita amekuwa mwanafunzi wa pili kitaifa kwa matokeo ya jumla. Msichana Grace Manga wa Shule ya Msingi Graiyaki ya mkoani Mara ametangazwa kuwa wa kwanza kitaifa katika matokeo ya mtihani huo.
Gwagi amesema kwa masomo ya sekondari anatamani kusoma katika shule za Ilboru, Mzumbe, Mpwapwa au Pugu kwa kuwa zimekuwa na matokeo mazuri.
Kwa mujibu wa mtoto huyo, wakati anasoma shule ya awali alirushwa darasa na kupelekwa darasa la pili kwa kuwa kila walipofanya mtihani alikuwa anaongoza.
“Na hapo sikuanza vibaya nilimaliza nikiwa number three (namba tatu) darasa la pili, nikaingia darasa la nne nikafanya mtihani wa Taifa, straight A in all the subjects (A kwenye masomo yote), mpaka naingia darasa la tano maendeleo yangu yalikuwa mazuri sana,” alisema Gwagi.
Aliongeza, “nimeshika number one standard six from January to Desember (kwa kwanza darasa la sita tangu Januari hadi Desemba), na mpaka naingia standard seven I have been number one from January to September (Darasa la saba wa kwanza tangu Januari hadi Septemba.”
CHANZO - HABARILEO
CHANZO - HABARILEO
Social Plugin