KUTANA NA KIUMBE HUYU WA AJABU... ANA JINSIA 720, HANA UUME WALA UKE,HANA TUMBO LAKINI ANAKULA

Kiumbe hicho ni miongoni mwa ajabu ya duniani


Hana mdomo , tumbo wala macho , lakini anaweza kutambua chakula na kukila. Hana mikono wala miguu , lakini anaweza kutembea na siku moja akaongeza ukubwa wake maradufu.

Anaweza kujifunza na kuwasilisha elimu yake kwa wengine bila ya kutumia akili. Anapokatwa katikati ana uwezo wa kupona kwa dakika mbili.

Wanasayansi wanajua kwamba sio mmea wala mnyama wala kuvu , ijapokuwa anafanana na wawili hao .

Na katika ulimwengu wake hakuna mume wala mke lakini jinsia 720 tofauti.

Kumbe hicho kinaitwa Physarum Polycephalum, ikimaanisha ukungu wa wengi maarufu 'blob' na atashirikishwa katika maonyesho katika bustani ya wanyama ya Paris mjini Ufaransa kuanzia wikendi hii.

''Blob ni mojawapo wa vitu visivyo vya kawaida vinavyoishi duniani hii leo'', alisema mkurugenzi wa bustani hiyo ya wanyama, Bruno David ambaye anamuona kiumbe huyo kama kitu cha ajabu duniani.

Kiumbe huyo amekuwepo kwa miaka milioni , na bado hajulikani ni kiumbe wa aina gani. Anatambulika vizuri kuwa mnyama , ama iwapo ni kuvu ama kitu chochote kati yao, aliongezea.
Mira al "blob" en acción.

Jina Blob linajiri kutoka kwa filamu ya sayansi ya mwaka 1958

The Blob , ilioigizwa na Kijana Steve Mcqueen ambapo kiumbe kwa jina Blob kinakula kila kitu mbele yake katika mji mdogo wa Pennsylvania, Marekani.

Je kiumbe hicho kikoje?

Kiumbe hicho kilikuwepo duniani miaka 500 kabla ya wanadamu.

Kwa kipindi kirefu alitambulika kama kuvu, lakini katika miaka ya 90 , utafiti ulimweka katika kundi la myxomycetes, au ukungu katika kifungu cha familia ya amoeba.

Umbo lake anafanana na Spongy anayeteleza na huwa na rangi ya manjano lakini pia wapo wenye rangi ya waridi, weupe na wekundu.Kiumbe hicho hupatikana katika maeneo yenye unyevu kama vile mashina ya miti

Ana seli moja mara nyengine ikiwa na viini tete vingi ambavyo vinaweza kufanana na DNA yake na kugawanyika.

Mara kwa mara hupatikana katika maeneo ambayo kuna uozo wa majani na mashina ya miti , maeneo mabichi na yenye unyevu.

Huonekana kana kwamba ametulia mahala pamoja lakini hutembea chini chini kwa kiwango cha sentimita moja kwa saa akitafuta chakula miongoni mwa kuvu, Spores, bakteria na wadudu.

Anaweza kufikiria

Tabia moja ya 'Blob' ambayo huwashangaza wanasayansi sana ni uwezo wake wa kuweza kufikiria.

''Anaweza kukariri, ana uwezo wa kubadilisha tabia , anaweza kutatua matatizo, anaweza kutafuta njia mbali na kuonyesha tabia kama za mnyama'', alisema David , mkurugenzi wa bustani hiyo ya wanyama mjini Paris.

Uchanganuzi wa kiumbe hiki ulisababisha kuelezea zaidi jinsi ujasusi unavyofanya kazi - wa aina yoyote baada ya utafiti kuchapishwa 2016.Blob wenye urefu wa hadi mita 10 wamekuzwa katika maabara

Wanasayansi walihitimisha kwamba Blob licha ya kukosa neva , anaweza kujifunza kutokana na uzoefu na kubadilisha tabia yake mara moja.

Katika vipimo vya maabara, wanasayansi walichunguza jinsi kiumbe huyo alivyozoea kupitia daraja jembamba .

Anapokutana na mwengine anaweza kusambaza maarifa aliyonayo.
Huonekana kama ambaye hana Uhai

Iwapo wageni watakaohudhuria maonyesho hayo katika bustani hiyo ya Paris wanataraji kuona kiumbe hicho kikitembea, huenda wakashangazwa kwa kuwa matembezi yake hayatabiriki.

Kabla ya maonyesho hayo bustani hiyo ya Paris itakuwa na onyesho la kanda ya video ya blob akitembea kwa kutumia vidole vyake kwa jina Pseudopods.Kanda ya video ya Blob katika maabara ya Paris

Lakini tabia ya kiumbe hicho zinavutia.

Kinazaa kupitia Spores ambazo zinakuwa watoto wa kiumbe hicho.

''Hana jinsia mbili tofauti , lakini ana jinsia 720 hivyobasi uzazi wake hauna matatizo'', anaelezea David.

Lakini kama spishi nyengine , maisha yake hutokana na utafauti wa maumbile ambapo kwa kiumbe Blob huzaliwa wakati viumbe viwili hukutana.Kiumbe hicho hakina sampuli ya uke na uume lakini jinsia 720

Je kiumbe hicho hujilinda vipi?

Wakati anapotishiwa Blob hujifcha na kujikausha. Hali yake huwa kama kitu kisichohai, alisema mtaalamu wa Blop Audrey Dussutour wa taasisi ya utafiti ya kitaifa nchini Ufaransa aliponukuliwa na shirika la habari la AFP.

Unaweza kumtia ndani ya microwave kwa dakika chache na maji machache na utashangaa kumuona Blob yupo hai akiwa tayari kula na kuzaa.
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post