MKUU wa wilaya ya Korogwe kulia Kissa Gwakisa akimkabidhi namba ya ushiriki mmoja wa wananchi wa wilaya ya Korogwe Noah Gondwe ambao wamejitokeza kuajiandikisha kushiriki mashindano ya Korogwe Mini Marathoni yatakayofanyika kesho Jumapili ambayo yameandaliwa na Mkuu huyo wa wilaya
MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wananchi waliojitokeza kujiandikisha kushiriki kwenye mashindano ya Korogwe Mini Marathon yatakayofanyika kesho Jumapili wilayani Korogwe
MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa katikati akiwa na baadhi ya wananchi ambao wamejitokeza kujiandikisha kushiriki kwenye mbio za Korogwe Mini Marathon ambazo zitafanyika kesho Jumapili wilayani Korogwe
MKUU wa wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa kushoto akiwasikiliza wanariadhaa ambao wamefika wilayani humo kutoka mkoani Arusha kujiandikisha kushiriki kwenye mashindano ya Korogwe Mini Marathon yatakayofanyika kesho Jumapili mjini humo
MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa aliyesimama katikati akiwa kwenye picha ya pamoja nao
MASHINDANO ya Riadha ya Korogwe Mini yanatarajiwa
kufanyika kesho Jumapili mjini hapa huku yakitumika kuhamasisha wananchi
kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura kwa ajili ya
uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu.
Mashindano hayo yameandaliwa na Mkuu wa wilaya
ya Korogwe Kissa Gwakisa
Alisema lengo kubwa ni kumuenzi baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere
ikiwa ni kutimiza miaka 20 ya kumuenzi lakini pia kuchangia maendeleo wilaya ya
Korogwe huku akitoa wito kwa wananchi wajitokeza waungane pamoja kushiriki
kwenye mashindano hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkuu wa
wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa alisema kwamba mashindano hayo watatumia muda
mchache ambapo wataanza saa kumi na mbili asubuhi mpaka saa mbili nusu asubuhi yatakuwa
yamemalizika.
Alisema pamoja na kumuenzi baba wa Taifa ambaye
alipenda demokrasi ya nchi yetu na ndio maana alipigania sana vyama vingi
kwenye nchi yetu na hadi kufikia kusema wachache wapewe mpaka hivi leo kuna
vyama vingi.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba mambo
makubwa aliyoyafanya Mwalimu Nyerere mpaka leo yanaendelea kufanywa na Rais aliyepo
madarakani Dkt John Magufuli kwa kuendelea kuenzi demokrasia ndio maana
alihamasisha nchi nzima watanzania waendelee kujiandikisha kwenye daftari la
kupiga kura kwenye uchgaguizi wa serikali za mitaa.
Alisema kwamba Rais Dkt John Magufuli alisema watu
wajitokeza kwa wingi kuiandikisha kwenye daftari la kupiga kura huku akieleza
kwamba watakaofika kwenye mashindano hayo watapewa hamasa ya kwenda
kujiandikisha na watatoa usafiri kwa wale ambao hawajiwezi.
“Sisi kama ofisi ya DC kwa wale ambao watakuwa
hawajiwezi ili tutawapeleka waende kujiandikisha Korogwe lakini pia Korogwe
Mini Marathon italeta hamasa kwa wananchi kujiandikisha na kujitokeza kwa wingi
kwenye kujiandikisha “Alisema
“Lakini pia niwaambie kwamba ile mvua au jua tutaendelea
kuhamasisha wananchi kujiandikisha tokea tuanze tumeona mafanikio Halmashauri
ya wilaya tayari juzi wamejiandikisha asilimia 42 hivyo ninaamini kwamba siku
zilizobakia tutavuka lengo ambalo tumewekewa “Alisema DC Kissa.
Naye kwa upande wake mmoja wa wananchi wa Mtaa
wa Mbeza wilayani Korogwe Magesa Luhoga alisema kwamba wao wamejiandaa vema
kushiriki kwenye mashindano hayo na kwamba atashiriki kwenye kilimota 10.
Alisema mashindano hayo ni jambo jema kwa
wananchi wa wilaya ya Korogwe huku akimpongeza Mkuu wa wilaya hiyo kwa kuandaa
mashindano hayo kwani yataimarisha maendeleo huku wananchi wakiimarisha miili
yao.
Hata hivyo kwa upande wake Bakari Nchimbi ambaye
ni meneja mauzo kampuni ya TBL alisema kwamba watashiriki kwenye mashindano
hayo ili kuunga mkono juhudi za mkuu huyo wa wilaya za kuhamasisha maendeleo
Hata hivyo naye kwa upande wake Noah Gondwe
ambaye ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Mnyuzi alisema kwamba watashiriki mashindano
hayo kwa kuhakikisha wanamuunga mkono Mkuu huyo wa wilaya.