MKUU wa wilaya Korogwe Kisa Gwakisa akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusiana Mashindano ya Riadhaa ya Korogwe Mini Marathon yanayotarajiwa kuanza kutumia vumbi Octoba 13 mwaka huu mjini humo ambayo yatatumika kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ikiwemo pia kuchangia maendeleo ya wilaya hiyo kulia ni Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano hayo Juma Mwajasho kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini Mary Chatanda na Afisa Tarafa ya Korogwe Michael John
Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano hayo Juma Mwajasho akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa,Mbunge wa Jimbo la Korogwe mjini Mary Chatanda na Afisa Tarafa ya Korogwe Michael John
MBUNGE wa Jimbo la Korogwe Mjini Mary Chatanda akizungumza kwenye mkutano huo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa kushoto ni Afisa Tarafa ya Korogwe Michael John
MKUU wa wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa katikati akimkabidhi medali za mashindano hayo Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano hayo Juma Mwajasho kulia kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe mjini (CCM) Mary Chatanda
MASHINDANO ya Riadhaa ya Korogwe Mini Marathon yanatarajiwa kuanza kutumia vumbi Octoba 13 mwaka huu mjini humo ambayo yatatumika kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ikiwemo pia kuchangia maendeleo ya wilaya hiyo.
MASHINDANO ya
Riadhaa ya Korogwe Mini Marathon yanatarajiwa kuanza kutumia vumbi Oktoba 13
mwaka huu mjini humo ambayo yatatumika kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere ikiwemo pia kuchangia maendeleo ya wilaya hiyo.
Mashindano
hayo yameandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa yakiwa na lengo la
kuibua na kuendelea vipaji vya vijana wilayani humo ikiwemo kumuenzi Baba wa
Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa alisema kipindi hiki
ni muhimu sana kutokana na kwamba watanzania wamempata Rais Dkt John Magufuli
ambaye anafafana na Baba wa Taifa ambaye amekuwa akifanya kazi kubwa ya kuwapa
watanzania maendeleo.
Alisema lengo
kubwa ni kumuenzi baba wa Taifa Nyerere ikiwa ni kutimiza miaka 20 ya kumuenzi
lakini pia kuchangia maendeleo wilaya ya Korogwe huku akitoa wito kwa wananchi
wajitokeza waungane pamoja kushiriki kwenye mashindano hayo.
“Wakati
tunaadhimisha kumbukumbu ya Baba wa Taifa letu sisi Korogwe kupitia Mashindano
ya Korogwe Mini Marathon sisi kama Korogwe tutakuwa tumetimiza jukumu letu la
kumuenzi baba wa Taifa kwa vitendo”Alisema DC Kissa.
Aidha
alisema kwamba watatumia mashindano hayo kuchangisha fedha kwa ajili ya kujenga
madarasa 70 ya magufuli ambayo wanahitaji wadau wajitokeza kuwasaidia kwenye
harakati hizo za kuhakikisha wanainua sekta ya elimu kwa kuondosha changamoto
zilizopo
“Tunawashukuru
sana Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ambaye ni mdau namba moja wamechangia
kwenye mashindano haya lakini pia wamewachangia milioni 30 kwa ajili ya ujenzi
wa madarasa nimeona kuna mwamko mkubwa kutokana na mashindano hayo sana lakini
pia niwashukuru wadau wengine akiwemo Mwekezaji wa Mkonge Gomba, Klabu ya Sas Cyclne
tunaamini kwa mchango wao tutafika mbalimbali sana “Alisema DC huyo
Pia alisema
kwamba wamejipanga kuhakikisha kunakuwa na mambo mazuri ambapo kutakuwa na kikimbia
kilomita 5 ambapo Mkuu huyo wa wilaya atakimbia ,Kilomita 5 watakimbia pia
walemavu kwa kutumia baiskeli na magongo huku akiwaomba wananchi wa Korogwe
ambao ni wenyeji lakini nje kuna mwamko mkubwa sana.
Mkuu huyo
wa wilaya aliwataka wanakorogwe kujitokeza kwa wingi huku akieleza kwamba
wameongea na hifadhi ya Mkomazi ili waweze kupeleka wanyama kwenye mashindano
hayo mahali yanapoanzia na yatakapokuwa yakiishia huku akiitaja Hotel ya Rocky
Excutive Lodge wamekuwa wadau wakubwa kwenye mashindano hayo.
Awali akizungumza katika mkutano huo Mbunge wa
Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Mary Chatanda alisema kwamba wao wameunga mkono
jambo hilo kwa ni jema wanawatangazia wananchi wajitokeza kwa wingi kwa kufanya
hivyo watakuwa wamejitendea haki wenyewe .
Mbunge huyo
alisema kwamba jambo hilo ni jema sana kwani kama alivyosema DC ni kupata fedha
kwa ajili ya kuchangia maendeeo huku akiwataka vijana wajitokeze kwa ajili ya
afya zao.
“Niwahamasishe
wananchi wa Korogwe mjini wajitokeze kwa wingi lakini pia wajasiriamali
wajitokeze kwa wingi waweze kuweka mali zao kwenye mashindano hayo ili waweze
kupata kipato kutokana na wanunuzi”Alisema.
Kwa upande
wake Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano hayo Juma Mwajasho alisema
kwamba mashindano hayo yatanzia kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu Korogwe na yatapita
njia ya Dar- Arusha hadi kwenye mzunguko njia ya kuelekea Handeni na Kurejea
yalipoanzia.
Alisema
kwamba pia kutakuwa na mashindano ya baiskeli kilomita 60,Kilomita 10 ya
kujifurahisha ikiwemo ya riadha ya Kilomita 10 na kiimota 5 ya kukimbia kujifurahisha huku
akiweka bayana zawadi zenye thamani ya milioni 2 kwa ujumla zitatolewa na
washiriki wote watakaomaliza kilomita 60 na 10 watapata medali.
Hata hivyo
alisema kwamba wanategemea kupata washiriki wengi kwenye mashindano hayo ambapo
zaidi ya washiriki 500 watashiriki kwenye mashindano hayo huku wengine
wakitokea nchi jirani ya Kenya ambao wameunganishwa kupitia Hifadhi ya Taifa ya
Mkomazi.