Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KUFANYA SANA MAPENZI KUNAPUNGUZA SIKU ZA KUISHI....BABU WA MIAKA 85 ATOA USHAURI


Manju Mstaafu James Makungu Sombi

Na Kadama Malunde - Kisesa

Imeelezwa kuwa unywaji pombe,kufanya sana mapenzi na ulaji mbaya unachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza siku za kuishi kwa binadamu.


Hayo yamesemwa na Mzee James Makungu Sombi aliyezaliwa mwaka 1934 katika kijiji cha Mwamanga wilayani Magu mkoani Mwanza wakati akizungumza na Malunde 1 blog leo Jumapili Oktoba 27,2019 nyumbani kwake Kisesa jijini Mwanza.

Mzee Sombi ambaye sasa ana umri wa miaka 85 na bado nguvu za kutosha anasema siri pekee ni kwamba aliepuka matumizi ya pombe,kuepuka kufanya sana mapenzi na kula vyakula vya asili.

“Vyakula vya asili vinajenga mwili vizuri kuliko hivi vyakula vya kisasa mnavyokula,ukifanya sana mapenzi unaharibu mwili wako,walau fanya mapenzi mara mbili au mara tatu kwa wiki hapo ndipo utajenga mwili wako vizuri na epuka kunywa pombe kali zikiwemo gongo,hizi zinaharibu mwili”,amesema Mzee Sombi.

“Ukiona umeanza kuzeeka unatakiwa uanze kufanya mazoezi mbalimbali ikiwemo kutembea ili kunyoosha misuli na utumie vyakula vya asili ikiwemo ugali wa mtama,uji wa ulezi”,ameongeza

Mzee Sombi ni miongoni mwa waanzilishi wa Makumbusho ya Kisukuma ya Bujora yaliyopo Kisesa jijini Mwanza,ni Manju mstaafu aliyebahatika kutembelea nchi mbalimbali za Ulaya akitangaza utamaduni wa Kisukuma akiambatana na Padri David Clement ambaye alitoa wazo la kuanzishwa kwa Makumbusho ya Bujora.

Mwaka 2005 Mzee Sombi alikaribishwa nchini Denmark kuonesha jinsi Wasukuma walivyokuwa wanamuomba Mungu kwa njia za asili kabla ya kuingia dini za kigeni.

Mzee Sombi ni Mtaalamu wa Masuala ya Utamaduni wa Kabila la Kisukuma,Wasiliana naye kwa namba  0755903972
Mwaka 2005 Mzee Sombi akitoa burudani ya Ngoma ya zeze nchini Denmark
Mwaka 2005 Mzee Sombi akitoa burudani nchini Denmark
Mzee Sombi akionesha namna Wasukuma walivyokuwa wanamuomba Mungu kabla ya kuja kwa dini za kigeni

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com