MBUNGE RWAKATARE AHIMIZA VIJANA KUBORESHA TAARIFA ZAO KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA


 Mbunge Wa Bukoba Mhe. Wilfred Muganyizi Rwakatare akizungumza katika kanisa la KKKT Ibura

Na Lydia Lugakila - Malunde 1 blog
Mbunge Wa Bukoba Mhe. Wilfred Muganyizi Rwakatare amewataka wazazi kuhakikisha wanawahimiza vijana wao kutumia vizuri muda uliobaki kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kuboresha daftari la kudumu la mpiga kura ili kuhakikisha kila aliye na sifa za msingi anatumia fursa hiyo ya haki kikatiba kupata viongozi wanaowahitaji kwa maendeleo ya taifa.

Mbunge Wilfred Rwakatare ametoa hamasa hiyo leo Oktoba 6, 2019 katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Mtaa wa Ibura manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera aliposhiriki katika ibada hiyo na kupewa nafasi ya kuwasalimia wakristo wa kanisa hilo.

Akiongea na wakristo wa kanisa hilo amewataka wazazi kutumia nafasi na muda mwingi kuwakumbusha vijana wao kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kuboresha daftari la kudumu la mpiga kura ili kuhakikisha kila aliye na sifa za msingi anatumia fursa hiyo kikatiba kupata viongozi wanaowahitaji kwa maendeleo ya taifa.

Amesema lengo la kuwakumbusha vijana ni kutokana na kwamba kundi hilo limekuwa likibaki nyuma ikilinganiswa na makundi mengine katika zoezi kama hilo muhimu.

Adha ametoa wito kwa wananchi kutumia siku chache zilizobaki kuhakikisha wamejiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura ikiwemo kufanya uboreshaji wa taarifa zao ili waweze kustahili kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao 2020. 

Hata hivyo ametoa pongezi kwa usharika huo kwa maendeleo ya kanisa hilo na kuongeza kuwa atakuwa nao bega kwa bega katika masuala ya kimaendeleo.

Ikumbukwe kuwa zoezi hilo la kuboresha daftari la kudumu la mpiga kura limeanza Oktoba 3 na litahitimishwa Oktoba 9,2019 mkoani Kagera.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post