Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JAMAA AJITUPA MAJINI AKIJARIBU KUVUKA BAHARI KWA KUOGELEA


Kizaazaa kilizuka katika kivukio cha feri Likoni kaunti ya Mombasa nchini Kenya baada ya jamaa kujitupa Bahari Hindi na kujaribu kuvuka kwa kuogelea. 


Baada ya kujirusha baharini, Timiza alianza kuogelea akielekea ng'ambo ya pili huku umati ukiachwa na mshtuko. 

Inasemekana kuwa Timiza alichukua hatua hiyo kufuatia kusitishwa kwa muda kwa kuhuduma za feri kufuatia mkasa uliotokea Jumapili, ambapo gari lililokuwa limewabeba mama na mwanawe lilidondoka na kutumbukia baharini.

Iliwalazimu wapiga mbizi kuchukua hatua ya dharura na kumuokoa kabla ya kumkabidhi kwa maafisa wa polisi.

Shughuli ya kuitafuta miili ya Mariam Kigenda na bintiye Amanda Mutheu imefikia siku ya nne bila mafanikio kutokana na utata ambao umeikumba oparesheni nzima.

Mariam Kigenda na bintiye Amanda Mutheu

Oparesheni hiyo imekumbwa na utata wa aina yake hususan baada ya mpiga mbizi wa binafsi aliyetafutwa na familia ya waathiriwa kujiuzulu kwa madai ya kuhangaishwa na Jeshi la Wana Maji. 

Jeshi hilo lilimshutumu Musa Sila kwa kutoa taarifa ya kupotosha kwa familia ya waathiriwa wa mkasa huo kuhusu oparesheni nzima inavyoendeshwa na kule iliko miili ya wapendwa wao. 
Chanzo - Tuko

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com