Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya kamati inayoshughulikia kuhamasisha na kuondoa mimea vamizi mkoa wa Arusha.
Na.Veronica Ignatus,Arusha
Serikali mkoani Arusha imeitaka kamati inayoshughulikia kuhamasisha, na kuondoa mimeavamizi ,kutoa elimu kwa kushirikiana na wataalamu kwa taasisi mbalimbali za serikali, ikiwemo mifugo,Kilimo,Mazingira na wizara ya Afya, mashuleni na maeneo mbalimbali ya jamii juu ya mimea vamizi wa gugu karoti.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega, kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ,kwenye siku ya maadhimisho ya siku ya gugu karoti na visumbufu vingine vya mazao mkoani Arusha ,iliyofanyika wilayani Arumeru ,katika Taasisi ya Utafiti wa viwatilifu kwa ukanda wa kitropiki (TPRI) Mkoani Arusha.
Kwitega amesema kuwa bila ushirikiano wa pamoja kati ya wataalamu, wadau wa maendeleo ,kazi hiyo haitakuwa na maana wala mafanikio ,hivyo kila mmoja analojukumu lakuhakikisha anafanyakazi kwa nafasi yake, ili elimu na uelewa iwafikie jamii kwa ujumla katika mapambano hayo.
Ametoa wito kwa Waandishi wa habari ambao ni wadau muhimu na jeshi la mianvuli, kutumia vyema kalamu zao kuhabarisha jamii juu ya gugu hilo vamizi ,kwa kutoa elimu kwa umma juu ya madhara na namana ya kuliangamiza gugu hilo.
Mwenyekiti wa Kamati uhamasishaji wa kudhibiti gugu hilo, Ndelekwa Kaaya amesema kuwa dhumuni la siku hiyo ni kuwahamasisha na kutoa Elimu ya uelewa kwa wadau wa kilimo,mifugo,mazingira,afya ya binadamu,viongozi wa dini,viongozi wa kimila taasisi za Elimu ,makundi maalum watafiti ,wanasayansi ,wafanyabiashara viongozi wa siasa wafahamu kuhusu madhara
na udhibiti wa Gugu karoti na visumbufu vamizi katika mkoa wa Arusha, na mikoa mingine ambapo kuna visumbufu vamizi.
Amesema katika siku hiyo mada mbalimbali zinazohusiana na ueneaji usambaaji na mbinu,njia za kuzuia na kudhibiti visumbufu vamizi zitatolewa na wataalam mbalimbali toka taasisi za serikali na sekta binafsi ili kujenga uelewa kwa jamii ya watanzania.
Amesema kuwa jitihada zilizofanywa na kamati katika harakati za kudhibiti gugu hilo ni pamoja na kushirikiana na taasisi binafsi ,zimeweza kufanya utambuzi wa visumbufu vamizi ,na kuainisha maeneo yalipovamia.
Ameinisha changamoto zinayoikabili kamati hiyo katika kutekeleza majukumu yake ni pamoja na ukosefu wa rasilimali fedha, kwaajili ya kuwezesha uhamasishaji wa kuzuia na kudhibiti visumbufu vamizi, ikiwemo kuwafikia wadau wengi katika maeneo yaliyovamiwa mkoani Arusha.
Aidha ukosefu wa vifaa vitendea kazi ,vifaa kinga vinavyotakiwa kutumika
katika zoezi la ung’oaji wa visumbufu vamizi haswa katika maeneo mbalimbali katika barabara za jiji la Arusha, ambapo ushirikiano mdogo kutoka kwa wadau wenyewe katika maeneo yaliyovamiwa na visumbufu vamizi likiwemo gugu karoti.
Mtafiti kitengo cha kidhibiti visumbufu vya mimea kutoka (TPRI)Ramadhani Kilewa amesema kuwa aina hiyo ya visumbufu vya wadudu na wanyama ni tatizo katika mikoa yote nchini Tanzania,ambapo maeneo mengi yaliyovamiwa ni mashamba ya mazao ,malisho ya
wanyama,Hifadhi za taifa ya Arusha ,Ziwa manyara , Serengeti na Ngorongoro,maeneo ya makazi ya watu ,maeneo ya kutunza na kusambaza nishati ya umeme ,mabwawa ya maji kwaajili ya matumizi ya binadamu na
wanyama.
Kilewa ameyataja madhara yatokanayo na gugu hilo kuwa ni pamoja na magonjwa ya aleji ya ngozi kwa binadamu na wanyama,kifua kinachobana (pumu)kwa binadamu,umasikini katika ngazi ya familia, kata ,wilaya na
mkoa.(pumu)kwa binadamu.
Kiuchumi gugu hilo linasababisha kupungua kwa mavuno ya mazao ya chakula na biashara,Athari katika biashara ya utalii na wanyama kushindwa kupita kwenye baadhi ya mimea vamizi,maziwa ya wanayama wanaofugwa kuwa na uchungu kwasababu ya sumu iliyomo katika mimea vamizi,upungufu wa malishio ya wanyama pamoja
madhara kwa afya ya udongo na uoto wa asili na uharibifu wa mazingira
Aidha asili ya gugu hilo kwamba ni Amerika ya Kusini,A.kati na A.Kaskazini maeneo ya Mexico, hapa nchini Tanzania liliingia mwaka 2010 limetokea nchini Ethiopia,ambapo mmea mmoja huweza kutoa mbegu 15,000 ,25,000-100,000 na zinauwezo wa kuzaa kila baada ya miezi 4,mmea mmoja unaweza kutoa miche kwa mara tatu,unauwezo wa kukaa
ardhini kwa miaka kumi.
"Zinaenea kwa njia ya upepo,utengenezaji wa barabara,upepo binadamu wenyewe,Asia Afrika,Visiwa ,Austaralia Afrika ya kusini,nchi zote za Afrika ya Mashariki wa Afrika zaidi ya 13,kwa Tanzania taarifa iliyopo ni mikoa mitano,inaathiri uoto wa asili,inazuia mbegu za mazao zisiote ,inasaidia uzaliaji wa wadudu,vimelea vya magonjwa kwenda kwenye mazao mengine,inzi weupe".Alisema Kilewa.
Social Plugin