Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAZIRI WA MADINI DOTTO BITEKO APOKEA JENGO LA KISASA KWA AJILI HUDUMA ZA WACHIMBAJI MADINI KAGERA


Jengo la kituo cha umahiri kwa ajili ya wachimbaji wa madini mkoani Kagera.
Waziri wa Madini Dotto Biteko akizungumza katika hafla fupi ya kupokea jengo hilo

Na Lydia Lugakila - Malunde 1 blog
Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko amepokea jengo la kisasa la kituo cha umahiri kwa ajili ya mafunzo na huduma mbalimbali za wachimbaji wa madini mkoani Kagera  lililokamilika tayari kwa huduma ya mafunzo mbalimbali ya wachimbaji wa madini ili kuiwezesha sekta hiyo pamoja na wadau kufanya kazi kwa uhakika na kuwa katika daraja la juu kiuchumi.

Waziri Dotto Biteko amepokea jengo hilo lenye ghorofa 3 lililoghalimu jumla ya bililioni 1.081 leo Oktoba 4,2019  eneo la Zam Zam Manispaa ya Bukoba.

Waziri Biteko amesema anatambua umuhimu mkubwa katika sekta ya madini na kuwa wachimbaji hao hawana budi kufuata agizo la Rais Magufuli alilolitoa toka alipoingia madarakani alipoitaka sekta ya Madini kubadilika wa kuhama katika uchimbaji wa kubabaisha na wa ujanja ujanja.

Waziri huyo wa madini amesema ili wachimbaji hao waweze kufanya kazi hiyo kwa uhakika ni lazima wafuate sheria ndipo waandaliwe mazingira ya kuwafanya wawe kwenye urasimu kwa kuwapatia maeneo ya kuchimba,ambapo amesema tayari Rais Magufuli alishatoa maelekezo ili kuwawezesha kufanya kazi katika mazingira bora.

"Kwa kutambua umuhimu katika sekta hii tayari jumla ya leseni 156 zimefutwa mkoani Kagera ili kuwapatia wachimbaji wadogo ambao wako tayari kuchimba madini wafanye kazi hiyo kwa uhakika utakaowawezesha kuishi daraja la juu katika sekta ya madini hivyo wachimbaji tumieni jengo hili kama nyenzo kwa kuleta madini yenu tutawahifadhia hapa na tutawafanyia uthamani’’, alisema Waziri huyo 

Amesema nchi hii ina zaidi ya leseni 33,000 ambapo leseni nyingi zilikuwa zimekaliwa na watu ambao hawaziendelezi,na ambao hawachimbi bali wamekuwa wakisubiri wachimbaji wadogo wagundue halafu waje kuwaondoa.

Biteko amewapongeza wakandarasi ambao ni SUMA JKT kwa kukamilisha ujenzi wa jengo hilo kwa wakati akieleza kuwa hapakutokea usumbufu wa aina yoyote kama ilivyo kwa wakandarasi wengine hapa nchini.

Biteko pia amempongeza Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Elisha Marco Gaguti katika kupambana vikali na watoroshaji wa madini ambapo mkuu huyo amemhakikishia Waziri Biteko kuwa udhibiti mkubwa utaendelea kufanyika katika kuzuia utoroshaji wa madini ili wachimbaji wadogo waweze kunufaika.

Kwa upande Gaguti amesema lengo lake ni kuona Kagera inakuwa mfano mzuri katika sekta ya madini ambapo ameahidi kushirikiana na wananchi  ili mkoa wake uwe mfano katika sekta hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com