RAIS MAGUFULI AMTUMBUA MKUU TAKUKURU

Rais Magufuli amemtumbua Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Mtwara, Stephen Mafipa kutokana na kukosekana kwake katika mkutano wa hadhara alioufanya katika Kijiji cha Chukuku kilichopo Masasi mkoani humo.

Akiwa Chukuku, wananchi walimueleza Rais kuhusu madai yao dhidi ya fedha wanazowadai vingozi wa chama cha msingi Amcos baada ya viongozi hao kutoweka na fedha hizo.

Baada ya kupata malalamiko hayo, Rais Magufuli alimuita Kamanda wa Polisi wa mkoa ambaye alieleza kuwa wanaendelea kuwatafuta watuhumiwa.

Jibu hilo lilionekana kutomfurahisha Rais Magufuli ndipo alipotoa siku tano kwa kamanda huyo kuhakikisha viongozi hao wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sharia.

“RPC nakupa ndani ya siku tano waliokula fedha za wananchi wa hapa wakamatwe na wapelekwe mahakamani, mshirikiane na Takukuru, kamanda wa Takukuru mkoa yuko wapi,” aliuliza Rais Magufuli bila kupata majibu

Kufuatia ukimya huo aliomba simu yake kutoka kwa wasaidizi wake ambapo alipewa na kumpigia Brigedia Jenerali Mbungo na kumuelekeza kumuondoa kamanda huyo wa mkoa na kumtaka ampeleke mtu mwingine kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.

“Brigedia Jenerali, nipo hapa Masasai, nimemuita Kamanda wako wa TAKUKURU hapa hayupo, nimemfuta kazi hapahapa. Sasa nakuagiza leo hii uteue Kamanda mwingine, aje hapa asaidizane na RPC kuwakamata hao wezi na kuwafikisha kwenye mikono ya sheria.

“Hatuwezi tukavumilia huu ujinga na siwezi kukubali wananchi wangu wakanyanyasika. nataka utekeleze mara moja,” alisema Magufuli wakati akitoa maelekezo hayo kwa Brigedia Jen. Mbungo kupitia njia ya simu ya mkononi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post