Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAHAKAMA KUU YA TANZANIA KANDA YA MBEYA YATENGUA HUKUMU YA MBUNGE WA MBEYA MJINI,JOSEPH MBILINYI (SUGU)


Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya leo tarehe 11 October 2019 imetengua Hukumu,Mwenendo na Kifungo alichohukumiwa Mbunge wa Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi aka Sugu kwa kile ambacho Mahahaka Kuu imeeleza kuwa ni ubatili wa mwenendo katika kesi hiyo. 

Akisoma Uamuzi wa Rufaa Nambari 29 ya Mwaka 2018 iliyowasilishwa na Sugu kupitia Mawakili Peter Kibatala na Faraji Mangula,Jaji Utamwa amesema kwamba kulikuwa na Makosa yasiyotibika katika mwenendo wa shauri hilo,hasa pale ambapo aliyekuwa Hakimu Mwandamizi Mteite wa Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mbeya aliposhindwa kuwasomea Mashtaka Washtakiwa katika hatua ya usikilizaji wa awali (Preliminary Hearing). 

Katika Hukumu yake iliyosomwa na Naibu Msajili wa Mahaka wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Jaii Utamwa alisema kwamba hakubaliani na hoja za upande wa Serikali ambao ni Wajibu Rufaa kwamba mapungufu hayo yanatibika, na badala yake Jaji Utamwa amesema kwamba makosa hayo yanaathiri mwenendo mzima wa kesi iliyopelekea kufungwa kwa Sugu na mwenzake Emmanuel Masonga.

Jaji Utamwa ametengua Hukumu, Mwenendo mzima wa kesi na adhabu ya kifungo waliyohukumiwa Sugu na Masonga.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com