MAHAKAMA YATAKA KESI YA ALIYEKUWA MHASIBU MKUU TAKUKURU ITENDEWE HAKI


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema haki itendeke katika kesi ya kumiliki mali ya zaidi ya Sh3.6 bilioni kinyume na kipato halali inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru),Godfrey GugaI na wenzake wawili kwa kuwa washtakiwa hao hawana dhamana.


Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba  ameeleza hayo leo Oktoba 21, 2019 wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi lakini upande wa mashtaka kupitia wakili wa Serikali Silivia Mitanto kudai kuwa kesi hiyo ilikuja kwa  ajili ya kuendelea na ushahidi lakini mawakili wanaosimamia kesi hiyo hawapo wapo mahakama ya mafisadi.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Simba alisema hajafurahi kuona kesi hiyo inaahirishwa kwani lazima waitendee haki  kwa sababu mashtaka yanayowakabili washtakiwa hayana dhamana.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 28 mwaka huu kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post