Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAKAMU WA RAIS KUFUNGUA MKUTANO WA MWAKA WA SHIRIKA LA MASHAURIANO YA KISHERIA KWA NCHI ZA ASIA NA AFRIKA (AALCO)


Eric Msuya – MAELEZO
Makamu wa Rais mama Samia Suluhu Hassan anatalajia kumuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa 58 wa mwaka wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO) utakoanza  Jumatatu tarehe 21 hadi 25 Oktoba jijini Dar es Salaam. 


Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga, amesema Mkutano huo utaudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali kutoka Nchi 48 za Wanachama wa Shirika hilo pamoja na Masharika mbalimbali ya Kitaifa. 


“Mkutano huu utakaoanza Jumatatu unatarajiwa kuhudhuriwa na Mawaziri, Wanasheria Wakuu wa Serikali toka Nchi Wanachama, Wawakilishi wa Mashirika mbalimbali ya Kimataifa, Mabalozi wanaowakilisha Nchi zao hapa Nchini na Viongozi Waandamizi wa Serikali kutoka Nchi Wanachama” Amesema Mhe. Mahiga 


Mkutano huo utaofanyika kwa siku tano, utajadili masuala mbalimbali ya kisheria za Kimataifa ikiwa pamoja na Changamoto za kisheria zinazoyakabili Mataifa Wanachama na Kuangalia namna bora ya kushughulikia changamoto hizo ili kuwa na Dunia yenye Amani, Usalama na Utulivu kwa ajili ya Maendeleo ya Kiuchumi, Kisiasa na Kijamii. 


Sambamba na hilo maswala mengi yatako jadiliwa katika mkutano huo ni, Sheria ya Kimataifa ya Bahari, Mitandao na Biashara na Uwekezaji, Kuvunjwa kwa Sheria ya Kimataifa Nchini Palestina, Utatuzi wa Migogoro kwa njia ya Amani, Matumizi ya Sheria za Nchi nje ya Nchi na Tume ya Sheria ya Kimataifa. 


Tanzania ilijiunga na The Asian – African Legal Consultative Organisation (AALCO) mwaka 1973 chini ya Uongozi wa Rais Hayati Baba wa Taifa  Mwl. Julius Kambarage Nyerere, huku Tanzania ikiwa ni mara yake ya tatu kuwa wenyeji wa kushiriki katika mkutano huu wa Shirika la Mashauriano ya kisheria kwa nchi za Asia na Afrika 


“Kwa mara nyingine tena, Tanzania tunakuwa wenyeji kwa mara ya tatu katika mkutano huu … Nchi yetu ina miaka 46 toka tujiunge na chama hichi, mafaniko ni mengi na maslahi ni makubwa na mapana tunayoendelea kuyapata katika chama hiki” Amesema Mhe. Mahiga 


Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika ( The Asian-African Legal Consultative Organisation – AALCO kilianzishwa  mwaka 1956 ikiwa ni matokeo ya Mkutano wa Kihistoria wa Bangung, Indonesia tarehe 18-24 April 1995 (Bandung Conference).


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com