Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Makamu wa Rais Samia Suluhu Awataka Wananchi Kujitokeza Kwa Wingi Kujiandikisha Ili Kuweza Kupiga Kura Serikali Za Mitaa

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la orodha ya mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu .
 
Akizungumza baada ya kujiandikisha kwenye daftari hilo katika Kituo cha Kujiandikisha Shule ya Msingi Kilimani illiyopo jijini Dodoma,Mama Samia amewataka watanzania kwa ujumla kujitokeza kujiandikindisha ili waweze kuchagua viongozi watakaowaletea maendeleo katika mitaa yao na kusisitiza wananchi kuchagua viongozi waadilifu na wenye uzalendo .
 
” Mimi leo nimeamua kutumia fursa hii kuja kujiandikisha katika mtaa wangu wa Salmini na najua ni haki yangu kuchagua Mwenyekiti wa Mtaa wangu na viongozi wangu kwa sababu najua makazi yangu hapo Dodoma na hawa ndio watakaosimamia mambo yangu kwenye mtaa wangu”amesema Mama Samia
 
”Hii ni fursa pekee ya kuhakikisha mnapata nafasi ya kumchagua kiongozi ambaye atasaidia kuleta maendeleo kwenye mtaa au kijiji chako kwa kipindi cha miaka mitano hivyo wakazi wote nawaomba mjitokeze kwa wingi kujiandikisha
 
Hivyo amewataka watanzania kuchagua viongozi waadilifu wenye kujali maslahi ya wananchi, wenye maadili ya kuwatumikia watanzania na wenye kutunza rasimali za wananchi wao na ambao watawasaidia viongozi wa ngazi za juu katika kuwatumikia watanzania.
 
Awali Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Benelith Mahenge,amesema kuwa  zoezi la uandikishaji ndani ya Mkoa huo limeanza jana na kwamba matarajio yao ni kuandikisha wananchi Laki Tisa.
 
” Idadi ya vituo ndani ya Mkoa wetu ni 3, 679 na toka jana tumeandikisha watu 156,000 hivyo tunaamini mpaka siku saba ziishe ambazo ni za uandikishaji tutakua tumezidi hata idadi kwa kuwa wananchi wengi pia wanaenda makazini hivyo siku za Jumamosi na Jumapili watapatikana kwa wingi,” Amesema Dk Mahenge.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com