Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, ametengua kauli ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, iliyokuwa inazuia watu kuabudu katikati ya juma kwa madai ya kuwa hawezi kuwapangia watu masaa na siku za kumuabudu Mungu wao wanayemuamini.
Kauli ya kutengua agizo hilo ameitoa leo Oktoba 22, 2019, alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake na kuwataka viongozi mkoani humo kuwa na kiasi hasa linapokuja suala la imani za watu na kwamba yeye anazihitaji ibada hizo katika mkoa wake.
''Upande wa imani Serikali haina dini, Natengua kauli ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala, watu wendelee kwa imani zao bila kuathiri sheria za nchi, viongozi tunapaswa kuwa makini tunapoingia kwenyeatika mambo ya dini, mambo ya dini ni mambo imani, mimi mwenyewe hapa ni mlokole hunipangii muda wa kusali'' amesema Makonda.
Aidha Makonda amewataka Wakuu wa Wilaya wote mkoani kwake, kuhakikisha wanakutana na viongozi waliochini yao ili kujadili njia na namna yakuleta ufumbuzi katika masuala ambayo hayako sawa, badala ya kutoa maagizo ambayo yataathiri imani za watu, kwani suala la ibada linahitaji moyo na utayari wa mtu binafsi.
Social Plugin