Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWANAMKE MBARONI KWA KUMDANGANYA MPENZI WAKE KUWA AMEZAA NAE ILI APATE PESA ZA MALEZI

Polisi katika eneo la Fort Portal nchini Uganda wanamshikilia mwanamke mmoja anayeshutumiwa kumtoa mtoto wake mchanga wa miezi mitatu kwa jirani yake mwanamke ili amdanganye rafiki yake wa kiume, limeripoti gazeti binafsi la The Monitor nchini Uganda/ Na URN.

Inadaiwa Annet Kobusinge alimdanganya 
mpenzi wake kuwa alizaa nae mtoto ili apate pesa za malezi ya mtoto

Mshukiwa huyo Annet Kabalisa, mkazi wa kijiji cha Kagote anadaiwa kumtoa mtoto wake mchanga kwa Annet Kobusinge ili kumlaghai kuwa mpenzi wake wa kiume Moses Musinguzi, ambaye alikuwa amemdanganya kuwa alikuwa mjamzito.

Msemaji wa mkoa wa Rwenzori Magharibi , Lydia Tumushabe, anasema kuwa Kobusinge, alimuomba Kabalisa kumchukua mtmto wake mchanga ili kumlaghai kuwa ni mwanae ili Musinguzi alipie gharama za malezi ya mtoto.

Kabalisa anaripotiwa kukubali pendekezo hilo na akamtoa mtoto kwa Kobusinge ambaye alisafiri usiku huo huo hadi Kampala.

Hata hivyo alipowasili mjini Kampala, Musinguzi anaripotiwa kutaka kubaki na mtoto huyo. Lakini baada ya kubaini kuwa mpenzi wake alitaka kubakia na mtoto, Kabalisa alitoroka hadi kwa kiongozi wa eneo hilo siku iliyofuatia na 'kuripoti kuwa mtoto wake mchanga ametekwa '.

Polisi wa Fort Portal walishirikiana na wenzao wa mjini Kampala na kubaini mahali alipo Kobusinge, mtoto mchanga na Musinguzi

Muhumuza ansema kuwa aliifahamisha polisi na wakazi wa eneo hilo ambao walingilia kati na kuanza kumsaka mtoto mchanga .

Hata hivyo katika 'mchakato wa kumtafuta ', mwendeshapikipiki(bodaboda) ambaye hakutajwa jina ilimfahamisha Muhumuza kwamba tayari amemsafirisha Bi Kobusinge na mtoto huyo mchanga hadi kwenye stendi ya mabasi ya abiria mjini Kampala na kumfikisha hadi kwenye kituo cha mabasi yanayokwenda Kmjini Fort Portal.

Hapo ndipo polisi walianza kumhoji Bi Kabalisa ambaye hatimae alielezea 'ukweli wote.'

Polisi walimkata mara moja Bi Kabalisa ili kusaidia uchunguzi. Jamaa watano wa familia pia walikamatwa na kuhojiwa baada ya kubainiwa kuwa wao pia walifahamu kuhusu mpango huo lakini hawakuripoti kwa polisi.

Polisi wa Fort Portal walishirikiana na wenzao wa mjini Kampala na kubaini mahali alipo Kobusinge, mtoto mchanga na Musinguzi.

Wawili hao pia walikamatwa na kushikiliwa katika kituo cha apolisi ambacho hakijafichuliwa.

Tumushabe amesema kwua Bwana Musinguzi amesema kuwa alimshikilia mtoto huyo mchanga kwasababu alitaka alipwe pesa zake zote alizotumia kugaramia mimba feki ya Kobusinge.

"Watu wamekuwa waliilaumu mara kwa mara polisi kwa kutojali visa vya aina hiyo huku vimekuwa vikisababishwa na watu wenyewe wanaojifanya kuwa ni walalamishi . Tumeamua kulivalia njuga swala hili hadi mwisho ," alisema msemaji wa polisi wa Fort Portal Tumushabe.

"Tuliwaonya watu kukoma kujihusisha na mipango ya uhalifu wa aina hii na tunawaomba waripoti visa vya aina hii," amesema
Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com