SHULE 10 BORA KITAIFA,MIKOA 10 ILIYOONGOZA,WATAHINIWA 10 BORA KITAIFA MATOKEO DARASA LA SABA 2019





Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 2019 ambapo asilimia 81.50 ya watahiniwa 933,369 wamefaulu mtihani huo huku watahiniwa 909 wakifutiwa matokeo kwa sababu ya udanganyifu.

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa leo Jumanne Oktoba 15, 2019 nafasi ya kwanza hadi ya 10 katika orodha ya wavulana waliofanya vizuri zimeshikwa na wanafunzi kutoka katika mikoa ya kanda ya ziwa.

Akitangaza matokeo hayo leo Jumanne Oktoba 15, 2019 Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk Charles Msonde amesema kwa jumla yanaonyesha ufaulu umeongezeka kwa asililia 3.78 lakini ufaulu katika somo la Kiingereza bado ni mdogo likilinganishwa na masomo mengine.

"Ufaulu katika somo la Kiingereza unaendelea kuimarika mwaka hadi mwaka hivyo juhudi za makusudi zinahitajika kuendelea kufanyika ili kuinua kiwango cha ufaulu katika somo hili," amesema Dk Msonde.

Aidha katika matokeo hayo, Grace Imori Manga wa shule ya msingi Graiyaki ya mkoani Mara ametangazwa kuwa wa kwanza kitaifa akifuatiwa na Francis Gwani wa shule ya msingi Paradise ya mkoani Geita na namba tatu imeshikiliwa na Loi Kitundu wa Shule ya msingi Mbezi ya Dar es Salaam.

Wengine katika orodha ya 10 bora ni Victor Godfrey wa shule ya msingi Graiyaki, Azizi Yassin wa Graiyaki goldie Hhayuma wa Graiyaki, Daniel Daniel wa shule ya msingi Little Mkoani Shinyanga, Hilary Nassor wa Peaceland ya Mwanza, Mbelele Mbelele wa Kwema Modern ya Shinyanga na Nyanswi Richard wa Graiyaki ya Mara.

Shule 10 bora kitaifa ni Graiyaki ya Mara, Twibhoki ya Mara, Kemebos ya Kagera, Little Treasures ya Shinyanga, Musabe ya Mwanza, Tulele ya Mwanza, Kwema Morden ya Shinyanga, Peaceland ya Mwanza, Mugini ya Mwanza na Rocken Hill ya Shinyanga.

Kimkoa, Mkoa wa Dar es Salaam umeshika namba moja ukifuatiwa na Arusha, Iringa, Kagera, Katavi, Kilimanjaro, Mbeya, Simiyu, Njombe na Pwani.

Halmashauri 10 bora zimeongozwa na Arusha jiji, Ilemela, Kinondoni, Mwanza jiji, Ilala Manispaa, Moshi Manispaa, Bukoba Manispaa, Iringa Manispaa, Biharamulo na Arusha

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post