Baraza la Mitihani la Taifa la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi ambako mikoa ya kanda ya ziwa imeonekana kuongoza.
Katika matokeo hayo yaliyotangazwa leo Jumanne Oktoba 15, 2019 nafasi ya kwanza hadi ya 10 katika orodha ya shule 10 bora kitaifa zimeshikwa na wanafunzi kutoka katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo mikoa ya Mara,Shinyanga,Kagera,Mwanza.
Kwa upande wa Watahiniwa bora kitaifa nafasi ya Kwanza imechukuliwa na mtahiniwa kutoka mkoa wa Mara,nafasi ya pili Geita, nafasi ya tatu mkoa wa Dar es salaam (siyo Kanda ya Ziwa),nafasi ya nne,tano,sita ni Mara, saba Shinyanga, nane Mwanza,tisa Shinyanga na kumi Mara.
Social Plugin