Mwanamke mweusi nchini Marekani ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi kupitia dirisha la chumbani kwake Jumamosi asubuhi , baada ya jirani yake kuiomba polisi iangalie hali yake.
Atatiana Jefferson, mwenye umri wa miaka 28, amekuwa akiishi katika makazi ya Fort Worth, mjini Texas na mpwa wake mwenye umri wa miaka minane.
Jirani yake alipiga simu kwa polisi wasio wa dharura baada ya kuwa na wasiwasi kwa kuwa mlango wa mbele ya nyumba yake ulikuwa wazi usiku.
Polisi wametoa picha za tukio , ambazo zinaonyesha afisa mmoja wa polisi akifyatua risasi dakika chache baada ya kumuona.
Picha hizo zinaonyesha polisi wakisaka makazi yake, baada ya kubaini umbo la mtu kwenye dirisha. Baada ya kumtaka mtu waliyemuona kunyoosha mikono juu, afisa mmoja wa polisi alifyatua risasi kupitia kwenye dirisha la kioo.
Idara ya polisi ya Fort Worth imesema katika taarifa yake kwamba afisa ambaye ni mzungu ''alihisi tisho" wakati alipoamua kumimina risasi.
Polisi huyo amepewa likizo huku uchunguzi ukiendelea , wamesema maafisa wa polisi.
Ufyatuaji huo wa risasi ulitokea majira ya saa nane na nusu usiku kwa saa za Texas.
Ingawa imefanyiwa uhariri video ya tukio inaonyesha maafisa wakijitambulisha kuwa wao ni maafisa wa polisi.
Picha hizo za video hata hivyo hazionyeshi ndani ya makazi , lakini zinaonyesha silaha ambayo polisi wanasema waliipata ndani ya chumba cha Atatiana Jefferson.
Haiko wazi ikiwa Bi Jefferson alikuwa ameshikilia silaha wakati huo, lakini kumiliki silaha ni kinyume cha sheria kwa watu wenye umri wa zaidi ya miaka 18 katika Texas.
Polisi wanasema maafisa walitoa huduma ya dharura ya matibabu kwa Bi Jefferson kwenye eneo la tukio , lakini alitangazwa kuwa amekufa kwenye makazi yake.
Bi Jefferson mwenye umri wa miaka 28 alikuwa akicheza michezo ya video na mpwa wake kabla ya kwenda kuangalia ni nini kilichokuwa kinasababisha kelele nje ya dirisha, kwa mujibu wa wakili anayeiwakilisha familia.Polisi wametoa picha ya silaha iliyobainika ndani ya chumba cha Bi Jefferson
"Mama yake alikuwa ameugua sana hivi karibuni , kwa hiyo akitunza nyumba na kufurahia maisha yao ," Wakili Lee Merritt alisema kwenye ukurasa wa Facebook. "Hapakuwa na sababu ya kumuua . Hakuna .Lazima tupewe haki."
Bi Jefferson alikuwa mhitimu wa chuo kikuu ambaye alikuwa akifanya kazi katika duka la mauzo ya vifaa vya maabara , aliongeza.
Ufyatuaji risasi huo umekuja chini ya wiki mbili baada ya afisa wa polisi aliyekuwa katika mapumziko kufungwa kwa kumpiga risasi mwanaume mweusi Bothan Jean, na kumuua katika makazi yake ya Dallas yaliyoko kilomita takriban 55 kutoka eneo la tukio la mauaji ya Bi Jefferson.
Mgombea wa urais kupitia chama cha Democratic Beto O'Rourke kutoka Texas amezungumzia kujusu kifo cha Bi Jefferson.
"Huku tukiomboleza kifo na wapendwa wa Atatiana, lazima tudai uwajibikaji na ahadi ya kupambana hadi wakati ambapo hakutakuwa na familia inayokumbwa na mkasa kama huu tena ," alituma ujumbe wake katika Twitter.
Chama cha Kitaifa cha maendeleo ya watu wenye rangi (NAACP) kimekitaja kifo cha Bi Jefferson kama "kisichokubalika".
Jirani aliyewaita polisi kwa jina James Smith, mwenye umri wa miaka 62, amesema kuwa binafsi aliangalia nyumba ya muathiriwa kabla ya kuwaita polisi , lakini hakuona kama kulikuwa na mtu ndani yake. but failed to spot movement inside.
"Ninatetemeka. Ninahasira. Nina jazba kubwa .Na ninahisi nikosa langu kwa kiasi fulani " Bwana Smith aliliambia gazeti la Star Telegram kuhusu ni kwanini aliamua kuwaita polisi waangalie hali yake . "Nisingewaita polisi kwa simu angelikuwa bado anaishi ."
Chanzo - BBC