Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 14 huko nchini Burundi amefariki dunia baada ya kupigwa na mwalimu wake, baba wa mtoto huyo ameiambia BBC.
Mtoto huyo, Chadia Nishimwe alipigwa viboko kwenye maeneo ya shingo na miguuni , kipigo ambacho kilimpelekea kutokwa damu puani na masikioni, alisema Jean-Marie Misago.
"Alikufa darasani mara baada ya kupigwa na mwalimu wake, na wakaenda kumtelekeza katika ofisi ya mwalimu mkuu," Bwana Misago alisema.
Mkuu wa shule alijaribu kumuwahisha hospitalini mtoto huyo wakati mtoto ameshakufa tayari, aliongeza baba huyo.
BBC imejaribu kutafuta taarifa zaidi katika sekta ya elimu bila mafanikio.
Mtoto huyo aliuwawa siku ya jumanne na kuzikwa siku hiyo hiyo .
Nchini Burundi, adhabu ya kuchapwa kwa mwanafunzi ni kinyume na sheria ingawa bado wanafunzi wanachapwa.
Social Plugin