Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya kazi,Vijana na ajira Anthony Mavunde wakati wa kufunga mafunzo ya ujasiriamali kwa Vijana yaliyofanyika mkoani Tanga
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi Beng'i Issa akizungumza wakati wa mafunzo hayo |
Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo
Serikali imesema itahakikisha
inaendelea kuliwezesha kwa ujuzi kundi la Vijana ili waweze kushiriki kwa
vitendo katika shughuli za kiuchumi na ujenzi wa Taifa
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya kazi,Vijana na ajira
Anthony Mavunde Leo wakati wa kufunga mafunzo ya ujasiriamali kwa Vijana
yaliyofanyika mkoani Tanga
Alisema kuwa kwa mujibu wa utafiti
wa nguvu kazi wa mwaka 2014 inaonyesha kuwa ukosefu wa ajira kwa Vijana ni
asilimia 11.7% duniani ambapo kitaifa ni asilimia 10.3%.
Hivyo kutokana na changamoto hiyo
serikali imeweza kuja na mikakati endelevu ya kuliwezesha kundi Hilo kupata
ujuzi wa kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali kwa ajili ya maendeleo
yao na Taifa.
"Tunatambua kwamba kikwazo
kikubwa kwa Vijana kushindwa kunufaika na fursa hasa za miradi ya kimkakati ni
kutokuwa na ujuzi stahiki ,hivyo kwa mafunzo hayo Nina imani yatakwenda kumaliza
changamoto ya ajira nchini"alisema Naibu Waziri Mavunde.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa
Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi Beng'i Issa alisema kuwa
mafunzo hayo ni muhimu kwa vijana kwani wanayahitaji kwa kutambua kuwa ujuzi
ndio msingi mkubwa wa maendeleo.
Alisema kuwa mafunzo hayo
yatawaongezea ubunifu na kutatua changamoto wanazokutana nazo katika shughuli
mbalimbali za kiuchumi wanazozifanya.
Mpaka Sasa jumla ya vijana 1,222
wamenufaika na mafunzo hayo katika mikoa ya
Dodoma,Ruvuma,Geita, Mwanza, Mbeya, Lindi na Tanga