Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe leo Jumatano, Oktoba 09, 2019 ataongoza makundi mbalimbali ya waombolezaji kuuaga wa aliyekuwa mtunzi wa na msanii nyimbo za Chama hicho, Fulgence Mapunda.
Mwili wa mwanamuziki huyo utaagwa katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Moyo wa Mtakatifu wa Yesu, Manzese, jijini Dar es Salaam, shughuli hiyo ya utoaji wa heshima za mwisho itaenda sambamba na salaam za rambirambi na pole kutoka kwa makundi mbalimbali.
Taarifa iliyotolewa na chama hicho imeeleza kuwa ibada ya kumuombea marehemu Fulgence Mapunda itakayofanyika kanisani hapo kuanzia saa 6 mchana, baada ya mwili kuchukuliwa kutoka Hospitali ya Mwananyamala ulikohifadhiwa, na baada ya hapo mwili huo utasafirishwa kwenda Ruvuma.
Mazishi yatafanyika siku ya Ijumaa, Oktoba 10, 2019, katika Kijiji cha Lituhi, Nyasa.
Marehemu Fulgence Mapunda alifariki Dunia majira ya saa 4 usiku siku ya Jumapili, Oktoba 6, mwaka huu, akiwa Hospitali ya St. Monica alipokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu.
Social Plugin