Mwakilishi wa Korea Kaskazini katika mazungumzo ya mpango wa nyuklia yaliyofayika nchini Sweden, Kim Myong Gil amesema majadiliano kati ya nchi yake na Marekani yamevunjika.
Mwakililishi huyo wa Korea Kaskazini amesema Marekani haijabadilika na wala haiko tayari kuacha tabia na mtazamo wake wa awali.
Kwa upande wake msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani, Morgan Ortagus amesema maoni ya Gil hayaakisi maudhui ya mazungumzo hayo.
Majadiliano kati ya mataifa hayo mawili ni ya kwanza, tangu Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Korea Kaskazini Kim Jong Un walipokutana mwezi Juni na kukubaliana kuanza tena mazungumzo baada ya majadiliano ya awali kukwama mwezi Februari mwaka huu.
Social Plugin