Mbunge wa Jimbo la Ndanda (CHADEMA) ambaye ni Mjumbe wa Kamati kuu na Mwenyekiti wa Kanda ya Kusini Mh Cecil Mwambe ametangaza nia ya kugombea nafasi ya uenyekiti wa chama hicho Taifa, akiahidi kuleta mabadiliko kadhaa katika chama hicho.
Chadema imepanga kufanya uchaguzi wake mkuu Desemba 18, mwaka huu.
Bado haijafahamika kama Mwenyekiti wa sasa Freeman Mbowe atagombea tena au hatagombea.
Uongozi wa Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ulimalizika Septemba 14 na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ilitoa siku saba zinazomalizika leo saa 9.30 alasiri wawe wamewasilisha maelezo kwa nini hawajafanya uchaguzi.
Social Plugin