Mwenyekiti wa MISA Tanzania Bi. Salome Kitomari, akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) unaofanyika katika Hoteli Royal Village - Dodoma, Tarehe 19 Oktoba 2019.
Afisa Mwandamizi wa NSSF Dodoma Bi. Pamela Mallya akielezea Bidhaa na shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mfuko huo wa hifadhi ya jamii pamoja na kujibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wanachama wa MISA Tanzania.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA) wakiuliza maswali mbalimbali na kutaka kupata ufafanuzi kuhusiana na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii NSSF na PSSSF ambao walikuwa ni wadhamini wa Mkutano huo Mkuu.
Bw. Victor Kikoti, Meneja Matekelezo kutoka Mfuko wa Hifadhi wa watumishi wa Umma (PSSSF) akielezea Bidhaa na shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mfuko huo wa hifadhi ya jamii pamoja na kujibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wanachama wa MISA Tanzania.
Mwanasheria na Makamu mwenyekiti wa Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA) James Marenga akiwakumbusha wajumbe na wanachama wa MISA Tanzania
kuhusiana na katiba ya Chama.
Katibu wa Bodi na Mkurugenzi Bw. Gasirigwa Sengiyumva (wa pili kushoto) akiwasilisha ripoti za utekelezaji wa mambo mbalimbali ya Taasisi, wakati wa Mkutano Mkuu wa wanachama wa Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika(MISA) Tawi la Tanzania, Dodoma
Wajumbe wa Bodi, Sekretarieti, na Wanachama wa MISA Tanzania pamoja na wadhamini wa Mkutano Mkuu wa MISATAN ambao ni NSSF, PSSSF na TANESCO wakiwa katika picha ya pamoja.
Social Plugin