Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KUTANA NA MREMBO KIKONGWE

Mrembo wa miaka zaidi ya 70 kutoka nchini Nigeria ameiambia BBC namna anavyotunza mwili wake

Abimbola Olayinka Idowu, ambaye anajulikana kama Segilola Grey, anasema kuwa hana siri yoyote inayomfanya kuendelea kuwa mrembo hata katika umri wake wa uzee.

Mzee huyo anasema kuwa huwa hafanyi chochote cha zaidi zaidi ya kuwa anafanana na mama yake, anakula vizuri na anapumzika.
Miaka mitatu iiyopita anasema kuwa mtoto wake alikuja na wazo la kumtaka awe mwanamitindo kwa kupiga picha cha mavazi mbalimbali.

Bibi huyo anasema kuwa anafurahia kufanya kazi hiyo na anaona kuwa ni jambo zuri kulifanya katika jamii.

Kama yeye mzee ameweza hata akina mama wadogo wanaweza pia, muhimu ni kujitunza na kupumzika vya kutosha.Segilola Grey anapenda kutangaza mavazi zaidi

Mtoto wake mwenye umri wa miaka 29 Tosin Idowu, anasema kuwa mama yake ni mrembo ndio maana aliamua kumtumia katika mradi wake wa picha.

Tosin Idowu a nasema kuwa ni jambo la kipekee kwa mama yake kufanya kazi hiyo na anaona kuwa watu wanampenda na wanapenda kazi yake nchini Nigeria.

Tosin anasema kuwa mpaka sasa hajawahi kupata lawama yoyote kwa kumtumia mama yake kuwa mwanamitindo.
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com