Eneo lililokumbwa ana mafuriko
Jumla ya watu 9 wakiwemo Wanafunzi watano wa Shule ya Msingi Nyachilo, wameripotiwa kufariki dunia kufuatia mvua kubwa, zinazoendelea kunyesha katika mkoa wa Morogoro.
Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Wilbroad Mutafungwa, ambapo amesema watu hao wamekufa maji katika matukio tofauti na sehemu tofauti, ikiwemo wanafunzi watano kusombwa na maji katika Mto Mvuha, wakati wakitoka shuleni, huku wawili wakielezwa kupoteza maisha baada ya kuzama katika Bwawa la kuhifadhia maji machafu ya miwa, linalomilikiwa na kiwanda cha Sukari cha Kilombero.
Kamanda Mutafungwa amewataja waliokufa katika matukio hayo kuwa ni Rajabu Issa, Shabani Msimbe,Neema Rajabu, Latifa Khalidi, Munira Khalid, Omary Khalidi ambao miili yao imepatikana huku mmoja wao Zainabu Rajabu, mwili wake bado haujapatikana.
Social Plugin