Mkurugenzi wa Mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA) Dkt Agnes Kijazi
Mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA), imetoa tahadhari ya mvua kubwa kwa siku mbili mfululizo, kuanzia Oktoba 17 na 18, 2019, katika mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani na Visiwa vya Unguja na Pemba, hali itakayopelekea kusimama kwa muda kwa shughuli za kiuchumi katika maeneo hayo.
Taarifa hiyo imetolewa leo Oktoba 16, 2019, na mamlaka hiyo kwa lengo la kuwatahadharisha wananchi hususani waishio mabondeni, ambapo athari hizo pia zinaweza kujitokeza Kaskazini mwa mkoa wa Morogoro.
Aidha taarifa hiyo imesema kuwa upo uwezekano wa mvua hiyo kutokea kwa wastani na kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na ucheleweshwaji wa usafiri.
Chanzo - EATV