Zaidi ya nyumba 20 katika kijiji cha Kamsanga B, kilichopo Kata ya Mnyagala Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, zimebomoka huku zingine zikiwa zimeezuliwa mapaa, kutokana na mvua iliyoambatana na upepo mkali na kujeruhi watu watatu.
Akizungumzia tukio hilo Mtendaji wa Kijiji hicho Mwikobe Saimon, amesema mpaka sasa nyumba 17 zimebomoka na nyumba 20 zimeezuliwa mapaaa.
"Jana majira ya jioni mvua iliyoambatana na upepo mkali ilianza kunyesha na ikaezua mapaaa na tulifika kuangalia namna ya kuwanusulu ila nyumba ishirini mapaa yake yalikuwa yamedondoka na nyumba 17 ndiyo zilikuwa zimebomoka kabisa" amesema Mtendaji wa Kijiji hicho Mwikobe Saimon.
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika, Salehe Mhando, amefika kijijini hapo na kutoa pole kwa waathirika wa upepo huo, ambapo amesema kuwa Serikali itaandaa utaratibu maalum wa kuwasaidia.
"Kwenye suala la ujenzi inabidi tuendelee kuelimishana ili tuweze kuweka vizuri, mfano nyumba ikiwa haijafungwa lenta ikipata misukosuko inabomoka" amesema Mkuu wa Wilaya.
Social Plugin