Naibu Waziri Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amewakumbusha Wazazi wenye watoto waliowapeleka kusoma katika shule binafsi wahakikishe wanawatimizia mahitaji yao ya muhimu katika kipindi chao chote cha masomo ili waweze kufaulu mitihani yao ya mwisho.
Badala ya kuja na zawadi nyingi siku ya mahafali ajili ya kuwapongeza wanapohitimu ilhali wanafunzi hao walikuwa wakirudishwa nyumbani kila wakati wakachukue ada ya shule.
Ametoa kauli hiyo jana wakati wa mahafali ya kidato cha nne kwa wanafunzi 60 yaliyofanyika katika shule ya Sekondari ya Rocks Hill iliyopo katika wilaya ya Ilemela jijini Mwanza.
Amesema wazazi lazima wawekeze kwa watoto wao ili waweze kusoma katika mazingira ya kutokuwa na hofu ya kurudishwa nyumbani kwa sababu wazazi wao hawajawalipia ada ya shule.
"Ukiamua kumsomesha mtoto lazima ukubali kwamba elimu haijawahi kuwa bure, hivyo ni jukumu la kila mzazi kukidhi mahitaji ya mwanae likiwemo suala la kumlipia ada kwa wakati." alisisitiza Kanyasu
Amesema ni vyema wazazi hao kutambua dhamana waliyonayo katika kuwandaa watoto wao kielimu badala ya kusubili hadi watoto warudishwe nyumbani.
Mhe.Kanyasu amesema kitendo hicho cha wanafunzi kurudishwa nyumbani kwa ajili ya ada kimekuwa kikiwarudisha nyuma kimasomo kwa vile wamekuwa wakikosa baadhi ya vipindi.
Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu amewataka wazazi kuendelea kuwalea watoto wao katika maadili mema ili wasiweze kuharibikiwaa mara baada ya kuhitimu masomo yao.
Kwa upande wake Meneja wa Shule hiyo, Meshak Mpalanga amesema katika kipindi chao chote cha masomo wamelelewa kimaadili hali itakayowasaidia kupambana zaidi katika kuyamudu maisha
Akizungumzia jinsi walivyoandaliwa kwa ajili ya mtihani wao wa mwisho, Amesema anatarajia idadi kubwa ya wanafunzi watafaulu na kujiunga na kidato cha tano.
NayevMwanafunzi bora katika masomo yote aliyetajwa katika mahafali hayo, Diana Titus amesema wamejianda vyema na wapo tayari kwa ajili ya mtihani wao wa mwisho.
" Tunawashuru walimu wote kwa kutulea na kutufundisha, tunaamini sote tutafanya vizuri mitihani yetu.alisisitiza Mwanafunzi huyo
Social Plugin