Ndege mpya ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) aina ya Boeing 787-8 5H-TCJ Dreamliner ipo katika hatua za mwisho nchini Marekani kuja nchini, ambako inaundwa.
Jana, ofisa wa kitengo cha habari cha kampuni ya Boeing, Jennifer Schuld alituma picha za ndege hiyo aina ya Boeing 787-8 na kueleza kuwa ipo kwenye majaribio.
“Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania imeanza majaribio ya kuruka leo. Ndege hii 787 inaitwa Rubondo Island,” aliandika ofisa huyo kwenye ujumbe alioutuma kwenye akaunti yake ya Twitter ikiwa sambamba na picha kadhaa za ndege hiyo.

Air Tanzania 787-8 5H-TCJ out for a taxi test at PAE today.— Jennifer Schuld (@JenSchuld) October 12, 2019
This 787 is named “Rubondo Island” pic.twitter.com/BoZmHDF6vP
Social Plugin