Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), limeyafuta matokeo ya watahiniwa 909, waliobainika kufanya udanganyifu katika Mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi na kuagiza mamlaka kuwachukulia hatua, wale wote waliohusika kufanya udanganyifu katika mitihani hiyo.
Taarifa hiyo imetolewa leo Oktoba 15, 2019 na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt Charles Msonde, wakati akitangaza matokeo ya Darasa la Saba kwa mwaka 2019, ambapo ufaulu umepanda kwa asilimia 3.78, ukilinganisha na mwaka 2018.
Aidha tathmini ya awali ya matokeo hayo imeonesha kuwa ufaulu katika somo la Kiingereza bado uko chini, ukilinganishwa na masomo mengine licha ya kuwa unaendelea kuimarika mwaka hadi mwaka na kwamba juhudi za makusudi zinahitajika ili kuinua kiwango cha ufaulu wa somo hilo.
Jumla ya watahiniwa 947,077 wa Shule za Msingi walisajiliwa kufanya mtihani huo, wakiwemo wasichana 495,937, sawa na asilimia 52.37 na wavulana 451,140 sawa na asilimia 47.63, huku watahiniwa wenye mahitaji maalumu wakiwa 2678 sawa na asilimia 0.23
BOFYA HAPA KUONA MATOKEO
Soma pia hizi↡↡↡↡
Breaking : ANGALIA HAPA MATOKEO YA MTIHANI DARASA LA SABA MWAKA 2019
KAULI YA UONGOZI WA SHULE YA LITTLE TREASURES BAADA YA KUSHIKA NAFASI YA NNE KITAIFA, YA KWANZA KIMKOA MATOKEO DARASA LA SABA 2019
Soma pia hizi↡↡↡↡
Breaking : ANGALIA HAPA MATOKEO YA MTIHANI DARASA LA SABA MWAKA 2019
KAULI YA UONGOZI WA SHULE YA LITTLE TREASURES BAADA YA KUSHIKA NAFASI YA NNE KITAIFA, YA KWANZA KIMKOA MATOKEO DARASA LA SABA 2019