James Makungu akizungumza na Malunde 1 blog nyumbani kwake Kisesa Mwanza
Na Kadama Malunde - Kisesa
Vijana wameshauriwa kubadili mfumo wa maisha ili kukabiliana na changamoto ya kupungukiwa nguvu za kiume hali inayowaathiri kisaikolojia na kushindwa kutimiza majukumu yao ya kindoa.
Ushauri huo umetolewa na Mzee James Makungu Sombi (85) ambaye ni mtaalamu wa masuala ya utamaduni wakati akiongea na Malunde 1 blog leo Jumanne Oktoba 29,2019 nyumbani kwake Kisesa jijini Mwanza.
Mzee Makungu amesema tatizo la vijana kupungukiwa nguvu za kiume limekuwa likiongezeka kila kukicha kutokana na vijana kupendelea kula vyakula vya kigeni ambavyo vingi vina kemikali zinazoathiri miili yao.
“Tatizo kubwa ni lishe,tunakula kemikali nyingi sana,hizi bia,soda,mboga tunazokula mfano kabeji,mchicha,chinese,nyanya,nyanya chungu na vingine vyote vinapuliziwa dawa,unakuta ng’ombe,kuku wanachomwa sindano za dawa siku mbili tatu wanakua kisha mnakula. Sasa kama kila kitu kina kemikali,kina sumu utapataje nguvu za kiume?”,alihoji Mzee Sombi.
“Jitahidini kula vyakula vya asili,muangalie vyakula ambavyo havijapuliziwa dawa,tumieni uji wa ulezi,mtama na kuleni kwa wingi karanga mbichi ni nzuri kwa afya,zilizokaangwa siyo nzuri sana”,alishauri Mzee Sombi.
Katika hatua nyingine Mzee huyo alishauri wazazi kuachana na tabia ya kuwavalisha watoto nguo za kubana kwani zinachangia kwa kiasi kikubwa kuharibu maumbile ya watoto wao.
“Nguo zinazobana pia zinachangia misuli kuregea na kufanya maumbo kuwa madogo ,nashauri pia vijana waache tabia ya kujichua ‘kupiga punyeto’ kwani inachangia kuregeza misuli yao matokeo yake wanakosa nguvu za kiume na kutengeneza vibamia bila kujua”,aliongeza Mzee Sombi.
Mzee James Makungu Sombi ambaye ni mkazi wa Kisesa Mwanza Manju Mstaafu wa ngoma za Kisukuma na ni miongoni mwa waanzilishi wa Makumbusho ya Kisukuma ya Bujora yaliyopo Kisesa jijini Mwanza.
Mzee Sombi ni Mtaalamu wa Masuala ya Utamaduni wa Kabila la Kisukuma,Wasiliana naye kwa namba 0755903972