Rais Magufuli amewataka viongozi kuacha malumbano yasiyo na tija na badala ya katika kuwahudumia wananchi wao ambao wamewapa dhamana kubwa ya kuwaletea maendeleo.
Magufuli amesema hayo leo Ijumaa, Oktoba 5, 2019 wakati akizungumza na wananchi a Songwe mara baada ya uzinduzi wa Barabara ya Mpemba – Isongolea mbapo Mbunge wa Ileje (CCM), Janeth Mbene alisimama na kusema Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo hana ushirikiano na viongozi mbalimbali na kusababisha changamoto katika utendaji.
Mbene amesema mkurugenzi huyo amekuwa hatoi ushirikiano kwa wenzake na hatekelezi majukumu yake ipasavyo na kwamba tatizo hilo limekuwa likielezwa kwa viongozi mbalimbali na pia mkoa umelifanyia kazi.
Akijibu tuhuma hizo, Rais Magufuli amesema ‘Kuhusu hili la mkurugenzi unajua kwa watu ambao hawaijui Ileje unaweza ukashangaa, sina uhakika kama dhambi zote hizo ni za mkurugenzi,” amesema na kuongeza
“Taarifa niliyonayo mimi, na Jafo (Waziri wa Tamisemi) ni shahidi kwamba huyu mkurugenzi saa nyingine anaacha kazi zake za ofisini anaenda kufundisha darasani.”
“Sasa mkurugenzi simtoi hadi nipate taarifa zangu mwenyewe, mkurugenzi uko hapa, sikutoi mpaka nipate information zangu mwenyewe, viongozi tuache kuchongeana haya ndiyo yanayotukwamisha,” amesema Rais Magufuli