Kituo cha huduma za pamoja kati ya Tanzania na Zambia kilichopo mpakani Tunduma kwa Tanzania na Nakonde kwa Zambia, kimefunguliwa rasmi na Marais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli na Edgar Lungu wa Zambia.
Baada ya kufungua kituo cha huduma kwa pamoja kati ya Tanzania na Zambia, Marais wa Tanzania Magufuli na Edgar Lungu wa Zambia kila mmoja ameingia kwenye chumba cha nchi yake ishara ya kuanza rasmi kwa matumizi ya kituo hicho.
“Niipongeze Wizara ya Fedha kwa kazi kubwa wanayoifanya lakini zaidi niwapongeze zaidi Mamlka ya Mapato (TRA)’ kwa mwaka huu wamevunja rekodi kwa ukusanyaji wa mapato. “Leo tumefungua kituo cha kihistoria cha kiuchumi na kimuungano kwa nchi zetu mbili za Tanzania na Zambia.
“Serikali ya Tanzania ipo tayari kushirikiana na Serikali ya Zambia kurudisha reli ya Tazara na kama kuna watu wanakwamisha Mimi nitumbue huku na Rais Lungu atumbue huko kwake.-Rais Magufuli