RAIS MAGUFULI AMKABIDHI NAIBU MKURUGENZI WA TAKUKURU RIPOTI YA MIRADI 107 YENYE DOSARI



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Naibu Kamishna wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo ripoti aliyokabidhiwa na kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa wakati wa hotubia yake kwenye sherehe za Kilele za Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere zilizofanyika katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu Mjini Lindi Oktoba 14, 2019
                                                                             
***
Rais   Magufuli amemkabidhi naibu mkurugenzi wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo ripoti ya miradi 107 iliyobainika kuwa na dosari.


Miradi hiyo ilibainika kuwa na kasoro ilipotembelewa kwa ajili ya kuzinduliwa na kukaguliwa katika mbio za Mwenge wa Uhuru zilizofikia kilele chake leo Jumatatu Oktoba 14, 2019.

Rais Magufuli amekabidhi ripoti hiyo leo katika maadhimisho ya kilele hicho na kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere yaliyofanyika mkoani Lindi.

Awali, kiongozi wa mbio hizo kitaifa, Mzee Mkongea Ally alimkabidhi Rais Magufuli ripoti ya miradi ya Sh90.28 bilioni iliyokutwa na dosari.

“Sogea hapa mbele nikukabidhi ripoti hii, zege halilali. Naikabidhi hii ripoti ukafanye ukaguzi kila ukurasa, kila nukta na ukachambue wale wote wanaohusika wapelekwe mahakamani. Usisite wapeleke mahakamani,” amesema Rais Magufuli wakati akimkabidhi Brigedia  Jenerali Mbungo ripoti hiyo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post