Rais Magufuli jana Oktoba 11, 2019 amezindua mradi wa umeme wa Megawati 132 mkoani Katavi ambapo alisema mradi huo utaokoa zaidi ya Sh5.5 bilioni zilizokuwa zikitumika kununua mafuta kwa ajili ya majenereta ya kufua umeme.
Awali, Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani alisema mradi huo ulianza Mei 2019 na unatarajiwa kukamilika Mei 2020.
Alisema mradi huo utagharimu Sh135 bilioni na ulianza kwa kujenga kituo cha kusambaza umeme kitakachofungwa mashine mbili za megawati 50 kila moja.
Social Plugin